Pichani
juu na chini ni wasanii wa moja kati ya vikundi vinavyoshiriki Tamasha la ngoma
za Asili za makabila ya watu wa Mkoa wa Mtwara la MaKuYa wakifanya onyesho la
Ngoma katika Uwanja wa Nangwanda Mjini Mtwara. Tamasha hilo la Siku mbili
limevuta hisia za wakazi wengi wa mji wa Mtwara.
Tamasha la Ngoma za asili la
makabila ya mkoa wa Mtwara Maarufu kama Tamasha la MaKuYa limeanza rasmi, huku
vikundi mbalimbali vya sanaa vikonyesha umahiri mkubwa katika kucheza ngoma za
asili za makabila yao.
Tamasha hilo ambalo mwaka huu
lilianza kwa maandamano kutoka katika viwanja vya mashujaa kwenda Uwanja wa
Nangwanda maarufu kama uwanja wa Umoja mjini Mtwara limevuta hisia za wakazi
wengi wa mji wa huo na vitongoji vyake ambapo licha kuwepo kwa jua kali lakini
watu waliendelea kumiminika uwanjani kushuhudia wasanii wakisakata ngoma
mbalimbali.
0 Comments