BAADA YA ZIARA YA IRINGA MBEYA TWANGA WARUDI DAR

 Kalala Junior akiwa jukwaani .
Kuoka kushoto ni Kiongozi wa bendi Luizer Mbutu na Msafiri Diouf wakika katika moja ya maonesho ya bendi hiyo. 
Wakali wa Muziki wa Dansi wa  hapa Bongo African Stars ‘Twanga Pepeta’  wamerudi jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza ziara ya maonesho  yaliyofanyika katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Ziara hiyo ya siku tatu  ilifanyika wiki iliyopita ambayo ilisababisha bendi kutokufanya maonesho yake ya jijini Dar es Salaam kama ilivyokuwa kawaida katika ukumbi wake wa nyumbani Mango Garden na Leaderds Club.Hivyo basi Jumamosi hii wataendelea na ratiba yao kama ilivyopangwa. Siku ya Ijumaa Septemba 22 watakuwa katika ukumbi wa Free Time Resort Ukonga.
Aidha siku ya Jumapili watamalizia ratiba ya burudani yao mchana Leaders Club Kinondoni na usiku watakuwa Mzalendo Club Millenium Tower Makumbusho.
Pia katika maonesho yake Twanga Pepeta wanatarajia kuitambulisha nyimbo mpya  iliyotungwa na msanii  Badi Bakule ‘Jogoo la mjini’ inayoenda kwa jina la ‘Mwenda Pole Hajikwai’  ambayo itakuwa ni nyimbo mpya na ya  sita  bendi hiyo.
Nyimbo nyingine mpya  ni ‘Shamba la Twanga’  iliyotungwa na Grayson Semsekwa, ‘ Walimwengu hawana jema’ uliotungwa na Jumanne Said au J4 lapova, ‘Mapambano ya Kipato’ iliyotungwa na Mwinjuma Muumini, ‘Ngumu Kumeza’ umetungwa na  Mirinda Nyeusi na ‘Nyumbani ni Nyumbani’  iliyotungwa na Kalala Junior. 

Post a Comment

0 Comments