MWANAMITINDO maarufu nchini, Flaviana Matata ameendelea kung’ara
katika fani hiyo baada ya kung’ara katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya
London, London Fashion Week.
Flaviana ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa shughuli hizo za maonyesho mavazi, aliwavutia sana wadau wa maonyesho hayo na kumfanya mwanamuziki nyota wa kike duniani, Stefani Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la Lady Gaga.

Mwanamitindo huyo aliwasisimua wadau wengi wa mitindo wakiwemo watu
maarufu duniniani na kuendelea kujizolea sifa na kutangaza jina lake na nchi
yake pia.
Flaviana amekuwa akishiriki katika maonyesho hayo tangu mwaka 2010, hata hivyo mwaka huu ameonyesha kukomaa zaidi na kuweza kutawala jukwaa hilo.
Maonyesho ya mavazi ya mwaka huu yaliwahusisha wabunifu wengi maarufu wa
mitindo ambapo mmoja wapo ni Vivenne Westwood Red Label ambaye anatamba
duniani.
Pamoja na kuwepo kwa mbunifu huyo, mbunifu Philip Treacy naye alifanya mambo makubwa katika maonyesho hayo yaliyozinduliwa na Lady Gaga.

Flaviana alipewa heshima kubwa ya kuvaa jaketi la mwanamuziki aliyekuwa
mfalme wa muziki wa aina ya Pop, marehemu Michael Jackson. Pia alivaa mavaz ya
wabunifu maarufu kama Mike Fast na Christopher Raeburn.
Kutokana na jinsi
alivyoweza kutamba katika maonyesho hayo, Flaviana alifanyiwa mahojiano na
gazeti maarufu duniani la Marekani, Wall Street Journal.
Flaviana ambaye ni Miss Universe Tanzania wa mwaka 2007, aliweza kuipromoti nchi yake katika maonyesho hayo kama alivyofanya katika mashindano ya Miss Universe ya mwaka 2007 kwa kushika nafasi ya sita kati ya warembo 10 walioingia fainali. Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kuona Flaviana anaendelea kufanya vyema katika fani hiyo

0 Comments