Bonzo (63) akitoa nasaha baada ya kumpiga bondia chipukizi james martin (22) ambae ni sawa na mwanae wa tatu upande wa kulia ni Ibrahim kamwe na kushoto ni Yasin Abdallah-Ustadh
Kampuni ya Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya mkurugenzi wake Ally Ommar inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa jiji la Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa Afrika mashariki yatakayopigwa siku ya Iddi mosi na Iddi pili.
Ally Omar’Mwazoa’ akikimuhakikishia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika na mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya iddi mosi katika ukumbi wa CCM , Said mundi wa Tanga atazipiga na Habibu pengo wa Dar es salaam katika kugombania ubingwa wa Taifa wa TPBC uzito wa super feather raundi kumi.
Jumanne Mohamed wa Tanga atazipiga na Ally Bugingo wa Dar es salaam uzito wa Light Weight raundi
kumi,katika uzito wa Super Fly Haji juma (Tanga) na Mwaite Juma wa Dar es Salaam watacheza raundi nane na mapambano mengineyo mengi ya utangulizi wa mabondia wa watakaotoka katika vitongoji mbalimbali vya jiji la Tanga.
Na siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi pia zuberi kitandula
wa Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi,jay jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka morogoro pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia
wakongwe wa tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi. mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za
kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa Afrika mashariki.
0 Comments