AL HAJ Shaaban Mintanga akiingia Mahakama Kuu katika kesi inayomkabili ya kuhusishwa na usafirishaji wa dawa za kuleva,habari kamili baadaye.
Mintanga akiwa na pingu mkononi.UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya inayomkabili Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) Alhaji Shaaban Mintanga umeshindwa kuleta mashahidi mahakamani hapo kwa kukosa fedha za kuwasafirisha.
Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Anselm Mwampoma alidai kwamba gharama za kuwaleta mashahidi watano kutoka nchini Mauritius ni Dola milioni 19 za Marekani kiasi ambacho serikali imeshindwa kumudu hivyo wanafanya uwezekano wa kupata sauti na picha zenye ushahidi (Video Conference).
Kabla Jaji anayeisikiliza Dk. Fauz Twahib kuiahirisha hadi Julai 16 mwaka huu mawakili wa utetezi wakiongozwa na Jerome Msemwa, walilalamikia kitendo hicho na kudai kwamba ni mpango wa Serikali kuhakikisha mteja wao anafia mahabusu kwa kufanya uzembe wa kuwafuatilia mashahidi.
Wakili Msemwa alidai mahakamani hapo kwamba wakili wa serikali anapokea maagizo ya kuchelewesha kesi hiyo kutoka juu (bila kufafanua juu kwa nani) kuja kuomba muda zaidi wakati sheria ipo wazi kwamba iwapo mashahidi hawatapatikana, upande wa ushahidi unapaswa kufungwa.
“Mtuhumiwa anateseka rumande kutokana na hali yake… anaumwa moyo huku akitaabika bila sababu za msingi ni bora mngetoa hukumu ya kifungo kuliko kumtesa hivyo inaonekana Serikali ipo juu ya Mahakama,” alisema wakili Msemwa.
Akijibu hoja hizo wakili wa serikali alipinga kupewa maagizo kutoka serikalini kwa kuwa mhimili huo upo kwa ajili ya wananchi hivyo usingependa kuona raia wake akisota rumande huku akifafanua kwamba Msajili wa Mahakama Kuu alisema hakuna fedha za kuwasafirisha mashahidi hao.
Kesi hiyo iliyofunguliwa Julai 4 mwaka 2008 ambapo hadi sasa haijaanza kusikiliza mashahidi wake.
1 Comments