Rais Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo May 20, 2012 alikaribisha kwa chakula cha jioni uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Washington na vitongoji vyake katika hoteli ya Ritz-Carlton jijini Washington DC. Uongozi huo, kwa niaba ya wanachama wake, ulimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mmoja wa Marais wanne wa Afrika walioalikwa kwa mara ya kwanza katika historia kuhudhuria kikao cha nchi tajiri duniani zijulikanazo kama G-8 katika makazi ya mapumziko ya Rais wa Marekani ya Camp David, Maryland. Rais wa jumuiya hiyo Bw. Iddy Sandaly alisema kwamba mualiko wa kuhuduhuria mkutano wa G-8 alioupata Rais Kikwete umeendelea kudhihirisha kwamba mataifa makubwa yanaheshimu msimamo wake katika kuendeleza kilimo cha kisasa na kuondoa njaa duniani, ambavyo ndivyo vilivyokuwa kauli mbiu ya mkutano wa Camp David.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waziri wa kilimo Injinia Christopher Chiza pamoja na Waziri wa kilimo wa Zanzibar Mh Suleiman Othman Nyanga, pamoja na balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Sinare Maajar. (Picha na Ikulu)
0 Comments