SUPER D ANZISHA PROGRAM YA KUTAFUTA MABONDIA KUMI BORA ITAKAYOANZA MAY 4


Kocha wa kambi ya Ngumi ya mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila,pichani kulia.
'Super D', ameanzisha programu maalum ya kuwafanyisha mazoezi mazito
mabondia wake.
Ameamua kuanzisha programu hiyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwa
na pumzi na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani.

Akizungumza leo, Kocha huyo alisema kuwa mabondia wake watashiriki
katika mashindano ya 10 bora yaliyoandaliwa na Kinyogoli Foundation
yatakayofanyika May 4.

Alisema kuwa mabondia hao watazichapa katika mpambano wa aina yake
utakaofanyika mwezi ujao katika Ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

“Nimeanzisha programu ya aina yake kwa ajili ya kuwajengea uwezo
mabondia wangu ili waweze kuwa na pumzi za kutosha katika mashindano
mbalimbali” alisema. Super D

Aidha aliongeza kwa kusema wanaomba wadhamini kujitokeza kusaidi vitu
mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mchezo huo wa masumbwi kwa
kuwapatia vijana maja ata zawadi ndogo ndogo za kuwatia moyo
mashindano hayo yatakayowashirikisha vijana mbalimbali katika uzito
tofauti yatakuwa na lengo la kuendeleza mchezo wa masumbwi Nchini

Mapambano yatakuwa mengi kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuja
kujiandikisha kushiriki siku hiyo alisema Super D

Post a Comment

0 Comments