MAMA YAKE KANUMBA ATOA WOSIA KWA SHIWATA

Na Peter Mwenda

MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven
Kanumba amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na M
(SHIWATA) leo  Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona
wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi.

"Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa ipendo na ushirikiano mlionesha kwa
familia yangu, naomba muendeleze ushirikiano mliokuwa nao wakati
mwanangu akiwa nanyi, endeleeni kushirikiana" alisema Mama Kanumba.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji wa Kanisa la Elim
Pentekoste Ilala Bungoni, Mchungaji Livingstone Mwaitela alisema
wasanii na familia ya Kanumba wasisononeke kwa sababu Mungu alimpenda
mtoto wao huyo zaidi.

Alisema wasanii waendelee kumkumbuka mwenzao kwa kubadili mambo
yasiyompendeza Mungu badala yake wajiandae kwa kufanya mambo ambayo
yanampendezesha na kujiweka tayari siku akiwaita wawe tayari.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema Kanumba alikuwa mwanachama
wao namba 648 akiwa mmoja wa waliojitokeza kutafuta eneo kwa ajili ya
kujenga nyumba za wasanii kutoka Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye
kufanikiwa kupata eneo Mkuranga.

Marehemu Kanumba alifariki Aprili 5, wakati akikimbizwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka nyumbani kwake
Sinza kufuatia ugomvi wa mapenzi na msanii mwenzake Elizabeth Michael 'Lulu'

Post a Comment

0 Comments