TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 8, 2011
Serikali imeruhusu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinazohusu timu za Simba na Yanga. Hata hivyo ruhusa hiyo ni ya mechi mbili kwa wiki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za VPL zenye maskani yake Dar es Salaam waliwasilisha tena maombi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kutumia uwanja huo kwa mechi za ligi.
Kutokana na uamuzi huo wa Serikali mechi ambazo sasa zitachezwa kwenye uwanja huo ni Ruvu Shooting vs Yanga (Septemba 10), Azam vs Simba (Septemba 11), Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), African Lyon v Yanga (Septemba 15), Azam vs Yanga (Septemba 18), Yanga vs Villa Squad (Septemba 21).
Nyingine ni Yanga vs Coastal Union (Septemba 24), Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25), Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 14), Simba vs African Lyon (Oktoba 16), Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19), Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20), Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), Yanga vs Oljoro (Oktoba 23), Yanga vs Simba (Oktoba 29) na Moro United vs Simba (Novemba 5).
TWIGA STARS , BANYANABANYANA 2-2
Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imetoka sare ya mabao 2-2 na Afrika Kusini (Banyana Banyana) katika mechi ya michezo ya All Africa Games (AAG) iliyochezwa leo Uwanja wa Machava jijini Maputo, Msumbiji. Banyana Banyana ndiyo iliyoanza kupata bao kabla ya Twiga Stars kusawazisha dakika ya 25 kupitia kwa Mwanahamisi Shuruwa. Banyana Banyana ilianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata bao la pili. Zena Khamis aliisawazishia Twiga Stars dakika 60. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja huo huo. Katika mechi yake ya kwanza Zimbabwe ilifungwa na Banyana Banyana mabao 4-1. Boniface WamburaOfisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikikisho la Soka Tanzania (TFF).
0 Comments