SASA BENDI YA THE AFRICAN STARS 'TWANGA PEPETA' KUKAMUA MSASANI CLUB KILA MWANZO WA MWEZI

 Msafiri Said Diouf akiwa jukwaani na wanamuziki wa bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta' usiku huu katika onyesho lao la kwanza la mwanzo wa mwezi ambapo  bendi hiyo itakuwa ikipiga katika ukumbi wa Msasani Club 'Makuti' kila jumapili ya mwanzo wa mwezi. imefahamiaka.
 Kushoto ni muimbaji wa Twanga Khadija Mnoga 'Kimobitel' na Diouf kulia..
 Muimbaji na mopambaji wa jukwaa la Twanga Janet Isinika akiwa jukwaani .
 Mmoja wa wanenguaji wa Twanga   anaitwa Fasha.
 Haya wadau hapa viuno viko huruuuuu kuvitazama.
 Mdau wa muziki wa dansi nchini.
 Greyson Semsekwa  Rapa na muimbaji wwa Twanga.
 
 
 Mandela leo alitoa kali ya mwaka kucheza shoo na magongo kma mlemavu wa viungo ambapo alikonga watu  na kuthibitisha kwamba yeye ni zaidi ya mtundu.
 Kushoto ni Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani gazeti la The Guardian Fred Ogot akishare jambo na Asha Baraka usiku huu katika ukumbi  wa Msasani Beach Club.
                                                                  Nikitafakari jambo.
 Mandela Sura Mbaya ambaye ni mnenguaji tishio kwa upande wa wanaume hapa akiachia nyonga zake tartiiibuu.
Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta' Asha Baraka kushoto akifurahia jambo na Mwendeshaji wa Blogu hii Khadija Kalili usiku wa leo ndani ya Msasani Beach Club.Asha amewaambia wanahabari kwamba bendi hiyo itakuwa ikitumbuiza  kila Jumapili ya mwanzo wa mwezi kwa makubaliano maalumu na wamiliki wa ukumbi huo. 
Nani kakwambia Mabindia hawapendi  muziki kushoto ni  Mada Maugo naye alikuwepo katika kukamilisha mzunguko wa mwisho wa juma akipozi na mpigapicha wa kujitegemea wa  blogu hii Peter 'Kingkiff'.
Muimbaji  kiraka wa bendi ya Twanga Charls Gabriel 'Charlz Baba'.

Post a Comment

0 Comments