MWANAMUZIKI siku nyingi Kasaloo Kyanga ambaye ni pacha wa mwanamuziki Kyanga Songa amefariki dunia jana katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo jana jijini Dar es Salaam , mmoja ya wakurugenzi wa bendi ya Njenje ambaye aliwahi kufanya kazi na marehemu wakiwa bendi Tuncut Almas, John Kitime, alisema, Kyanga mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) alifariki baada ya kuugua. Kyanga aliingia nchini mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kutua bendi ya Super Matimila, kabla ya bade kujiunga na Orchestra Tomatoma na baadae Marquis De Zaire na Tuncut Almasi iliyokuwa na maskani ya Mkoani Iringa.
Akiwa na Marquis alifanikiwa kutunga na kuimba nyimbo kadhaa na wimbo uliompa umaarufu ni ‘Kalubandika’ kabla ya baadae kuitosa bendi hiyo na kuwika na Tuncut kwa nyimbo kama ‘Masafa Marefu’, ‘Nimemkaribisha Nyoka’, ‘Kashasha’ na nyinginezo. Marehemu ameacha mjane na watoto sita ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Sinza.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MALI PEMA PEPONI AMIN.
0 Comments