Pichani juu ni timu nane zenye watu wawili wawili kila timu ambazo zimeshinda kwenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya vipaji katika soka. Washindi hao wanatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini na kinywaji cha Guinness, toka kampuni ya SBL Tanzania.
Mashindano ya vipaji vya mpira ya ‘Guinness Football Challenge’ yamemalizika jana katika viwanja vya Leaders na kupatikana timu nane za watu wawili wawili kila timu ambao wanatarajia kupelekwa nchini Afrika Kusini kujiunga katika shule maalumu ya vipaji vya mpira wa miguu. Mashindano hayo ambayo yamezaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) chini ya kinywaji chao cha Guinness yalifanyika jana ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
0 Comments