MAPATO STARS Vs ALGERIA
Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.VIP A ambapo ndipo kulikuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000 .Jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu ambapo kiingilio kilikuwa sh.5,000 mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh.7,000 viti vya rangi ya chungwa sh.10,000 VIP C na sh.20,000 VIP B.
Bnoniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF).
0 Comments