Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.Unaweza kuwasiliana na Meneja wa Twiga Stars kwa nambari +258 840207262
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira Tanzania TFF.
0 Comments