Mwenyekiti wa Old Skul ambaye pia ni mwanamuziki wa bendi ya The Kilimanjaro 'Wananjenje' akionge katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani mchana wa leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mchana kuhusu muungano wa wanamuziki wazamani na sasa.Kushoto ni Le Maesto King Kikii na kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Fleva Unit 'TFTU' Hamisi Mwinjuma 'Mwana Fa'
Wajumbe kutoka Tanzania Fleva Unit TFU Banana Zorro Said Fella wakifuatiwa na Le Maestro King Kikii.
HAIJAWAHI kutokea nchini wanamuziki wa zamani na wa kizazi kipya kuungana katika jukwaa moja.
Wasanii hao wameungana katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yatakayofanyika baadaye mwaka huu.Imefahamika kwamba wanamuziki wa zamani watapanda jukwaani na kuimba nyimbo za wanamuziki wa sasa kadhalika wanamuziki wa sasa nao watapanda jukwaani na kuimba muziki wa zamani.Hakika itakuwa burudani ya aina yake kwa mashabiki na watanzania kwa jumla, kwani muziki utakaotoka hapo utakuwa na ladha ya ina yake,” anasema Mwenyekiti wa Oldskul, Waziri Ally.Kama hiyo haitoshi, naye mkongwe, King Kikii, ameahidi kufanya makubwa huku wakisisitiza kwamba mazoezi yanatarajiwa kuanza mapema wiki ijayo.Wanamuziki hao ambao wameonyesha njia na lengo la kuleta mapinduzi na mshikamano miongoni mwa wanamuziki hao wa Watanzania.Waziri anaongeza kwa kusema kuwa katika tamasha hilo la maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Uhuru, watawaonyesha wanamuziki wa sasa kwamba wao wanaujua ujana na uzee pia, huku wanamuziki wa sasa wakiwa wanajua ujana na si uzee.“Sisi wote tuna lengo moja la kuungana na kupanga nini tunataka kufanya katika tamasha hili la Miaka 50 ya Uhuru, itakayorindima Diamond Jubilee,” anasema Waziri.Anaongeza kwa kusema kuwa tamasha litakuwa na wanamuziki mchanganyiko, pia wako katika mchakato wa kufanya kazi pamoja miongoni mwetu sisi wa zamani na hawa wanamuziki wa kizazi kipya.Kwa umoja wao wanasema wote walikuwa wakiogopana nani aanze. Wanamuziki wa zamani waliona hawa wa sasa kama wana ujana sana, hivyo siku moja walivunja ukimya na kuweka wazo la kufanya kazi pamoja mezani, ambalo limezaa matunda. Hivyo, umoja huo utaonyesha matunda yake Desemba 8 ambapo ni mkesha wa miaka 50 ya Uhuru.Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya (Tanzania Fleva Unit TFU), Hamisi Mwinjuma, anasema kuwa itakuwa burudani ya aina yake siku hiyo kumsikia gwiji, Wazi Ally, akiimba wimbo wa ‘Dushelele’ wa Ali Kiba.“Na itakuwa vipi kama Banana Zorro ataimba kama galacha, King Kikii” anasema Mwana Fa.Naye mjumbe wa TFU, Said Fella, anasema tumepokea kwa mikono miwili wazo hili la kufanya kazi kwa kuchanganya umri. Hivyo, japokuwa kundi hili si rasmi tumekutanishwa na maadhimisho haya ya Miaka 50 ya Uhuru.Waziri anaongeza kwa kusema kuwa katika mkesha huo wameteua kuimba nyimbo zilizotamba kati ya mwaka 1961 na 2001.“Tutapanda kwa pamoja jukwaani siku hiyo. Mazoezi yataanza hivi karibuni, wadau na mashabiki wote wajitayarishe kuona jinsi nchi ya Tanzania ilivyojaliwa vipaji vya muziki”.Anamalizia kwa kusema kuwa tamasha hilo lina kaulimbiu isemayo, ‘50 years Old 50 Years Young’
MHE. KITANDULA ATOA WITO TANAPA KUITUNZA MIRADI YA REGROW MIKUMI
-
Zainab Ally – MIKUMI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, leo Januari 9,
2024, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ina...
30 minutes ago
0 Comments