Hey mambo sistaa Khadija, natumai unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku... Naitwa kijah mimi ni mmoja kati ya wafuatiliaji wa Blog yako lakini pia napenda kukujulisha kuwa nina blog yangu ambayo inaitwa afrokija, inayozungumzia hasa masuala ya muziki na wanamuziki Barani Afrika na ninalenga hasa yale yanayojiri kwenye kipindi changu cha Afrobeat kinachorushwa na East Africa TV kila jumamosi saa 1 jioni, ingawa pia napost na habari zingine zinazonigusa ambazo naamini watu wengine wangependa kuzifahamu. Hivyo naomba uwafahamishe wapenzi wa blog yako kuwa kuna hii blog ili waweze kupata habari za wanamuziki wa Afrika kupitia blog yangu(afrokija)
Natumai utanipa ushirikiano
Nakutakia kazi njema na Mfungo mwema.. Ramadhani Kareem.
Maneno kutoka kwa Sistaa Khadija "Hey Kijah nakupenda pia na hata mimi nakufuatilia sana kazi zako zinapendeza huna muda mrefu katika fani lakini uko saafii.Karibu mwanablogu mpya."
0 Comments