Social Icons

Sunday, July 10, 2011

WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAPAGAWA VILIVYO NA SERENGETI FIESTA 2011

WAKAZI Jiji la Mbeya hasa wale wadau na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, juzi walijitokeza kwa wingi katika kusherehekea Msimu wa Dhahabu kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2011, lililofanyika kwenye uwanja wa Sokoine, mjini hapa.
Kujazana kwa mashabiki hao waliokuwa na shauku kubwa ya kuona wasanii mbalimbali,ambao wote walikonga nyoyo za mashabiki na hata wakati ulipofika kwa hitimisho la tamasha waligoma kutoka Uwanjani kwa kile kilichoonekana muda kuwa mfupi ambapo walihitaji tamasha hilo liendelee.
Tamasha la Serengeti Fiesta lilianza muda wa Saa sita mchana na kuhjitimisha safari yake ilipofika saa 12:30 jioni.
Aidha tamasha hili limeandaliwa na Kampuni ya Prinme Time Promotions kwa kushirikiana na Clouds Media Group na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Wasanii waliofunika pamoja na kundi la Wanaume Halisi lililoongozwa na Juma Kassim ‘Nature’ ambao walivutia kwa nyimbo zao nyingi za zamani na hata namna ya uchezaji wao wa miondoko ya Mapanga Shaa ambapo uwanja mzima mashabiki walicheza nao na kwenza nao sambamba.
Wasanii wengine waliotia for a ni pamoja na Kundi la Gangwe Mob linaloundwa na Inspekta Haroun na Luteni Kalama, Mwana Fa, Profesa Jay, Kalapina, Jafffarai na Belle 9.
Wasanii wengine waliopagawisha mashabiki wa muziki wa mjini hapa ni pamoja na Joh Makini, Darasa, GodZila, Dayna pamoja na kundi la Tip Top ‘Connection’ likiongozwa na Madee na Tundaman waliofunika na wimbo la ‘Starehe gharama’ pamoja na ‘Bado Tunapanda’ ambazo zilionekana kuwapagawisha zaidi mashabiki wa muzki wa mjini hapa.
Tamasha ilo la Fiesta linalofanyika katika mikoa kumi ya Tanzania bara na mwishoni mwa wiki hii litarindima Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Arusha na Kilimanjao
Junior .


Dizzo One.


Belle 9.






Jaffarai.




Top C, wadau picha nyingine nyingi baadaye mtandao unamabariidii.

John Bukuku mwendeshaji wa Blog ya Fullshangwe akiwa katika pozi.

Jamani Mbeya Baridi wee acha tuu na hasa kwa sisi tuliozoea Majotroo mbonaa tumekomaa.


Kazi za kupandisha kazi katika blog zikiendelea.

Mkuu wa Ulinzi kutoka Kampuni ya Bia Serengeti John.

1 comment:

Anonymous said...

Good taswiraz Khadija Kalili. Tumepata burudani sana kwa muda wako uliokuwa mbeya. Ubarikiwe sana kama siku ya ufunguzi wa kiwanda cha bia moshi.

 
 
Blogger Templates