Semina na mitihani ya utimamu wa mwili (Physical Fitness Test) kwa waamuzi wa daraja la II na III iliyopangwa kufanyika Agosti 2 hadi 5 mwaka huu katika vituo vya Dodoma, Mwanza na Ruvuma imeahirishwa.
Hivyo waamuzi wote waliotakiwa kushiriki katika semina hiyo ambapo pia watajitegemea kwa usafiri, chakula na malazi wanatakiwa kusubiri hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine.
Semina na mitihani hiyo itakwenda sambamba na shughuli ya upandishaji madaraja kwa waamuzi ambao watafaulu. Hivyo tarehe nyingine ya semina itakapopangwa, wahusika wataarifiwa mara moja.
Nayo kozi kwa ajili ya watathimini wa waamuzi (referees assessors) inayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 30 hadi 31 mwaka huu.
Watathimini 20 wa waamuzi watashiriki kozi hiyo itakayofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wote ni waamuzi wastaafu.
Washiriki ni Alfred Rwiza, Charles Mchau, Charles Ndagala, David Nyandwi, Emmanuel Chaula, Hafidh Ally, Isabela Kapera, Joan Minja, Joseph Mapunda, Juma Ali David, Kapteni mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Manyama Bwire, Mchungaji Amy Sentimea, Mohamed Nyama, Omari Kasinde, Paschal Chiganga, Riziki Majala, Soud Abdi na Victor Mwandike.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Uwanja wa Gombani
Pemba leo 12-1-2025
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali
Mwinyi akipokea Maandamano ya Wananchi katika Maadhimisho ya Kilele cha
Miaka 61...
5 hours ago
0 Comments