LUDACRIS AWAPA RAHA WATANZANIA KATIKA SERENGETI FIESTA 2011

 Ludacriss  akiwa Jukwaani ambapo kila mtu aliyeingia katika viunga vya Leaders Club aliweza kumwona vyema  na kufurahia burudani yake aliyoitoa sauti nguvu  za kutosha  na kulimudu jukwaa ipasavyo.Kwa mdomo wake Ludacriss amekiri kwa kusema amejisikia raha na heshima ya aina yake  kwa kuja Tanzania ilhali yeye asili ya mtu mweusi na tayari amesha wapa majoto  mashabiki wake katika nchi za Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini na sasa leo ni zamu ya Tanzania.(Picha na uillshangwe.blogspot.com)
 Ludacriss  kulia akiimba sambamba na msanii mwenzake JZ katika kilele cha Serengeti Fiesta 2011  katika tamasha lililohudhuriwa na mamia ya mashabiki  na wamenda muziki  kutoka  kila kona ya jiji la Dar es Salaam , mikoa jirani na hata nchi jirani .
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) Richard Wells akiwa katika tamasha hilo  usiku wa kuamkia leo na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ephraem Mafuru.
 Raisi wa Masharobaro akitoa burudani.
 Sehemu ya umati wa  mashabi waliojitokeza kwenye tamasha  la Serengeti Fiestaa 2011 Leaders Club Dar.
Aidha mbali ya  watuwengi kujitokeza pia kulitokea tukio la aina yake la kuwashukuru waasanii waasisi wa Bongoflava.Kutokana na kwamba Tamsha hilo la Serengeti Fiesta limefanyika kwa mara ya kumi usiku wa kuamkia leo uongozi wa Kampuni za Prime Time Promotion na Clouds FM wamewapa tuzo baadhi ya wasanii ambao ndiyo walikuwa msingi wa muziki wa Bongo Flava nchini waliopata tuzo za heshina na kutambua mchango wao ni  Kundi la East Coast Team, Mandojo & Domokaya, Dully Sykes, Juma Nature,Mr. Nice,Profesa Jay,Lady Jaydee,Unique Sisters, Bushoke na  Fid Q.
 Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Bia Serengeti Ephraim Mafuru na Meneja wa Bia ya Serengeti Allan Chonjo.
 Msanii Chid Benz akiwa katika mahojiaono na Clouds TV.
 Gerald Hando (Clouds Radio), Khadija Kalili na Antonio Nugas (Clouds TV &Clouds bRadio).

Post a Comment

0 Comments