African Stars Entertainment imemkabidhi Mwanamuziki mkongwe Nchini Muhidin Ngurumo wa Msondo Ngoma Music Band kiasi cha shilingi Milioni mbili za kitanzania zilizokusanywa kutokana na onyesho lililofanyika Jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Mango Garden.
ASET Iliandaa onyesho hilo kwa lengo la kutafuta fedha ili kumchangia Mwanamuziki huyo kwa ajili ya kugharamia matibabu anayoendelea kuyapata pamoja na kujikimu. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mzee Ngurumo na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiongozana na meneja wa Msondo Ngoma Music Band Said Kibiriti na Meneja wa ASET Hassan Rehani nyumbani kwake Mzee Ngurumo Mabibo Makuburi.
Mara baada ya kukabidhiwa Mzee Ngurumo alitoa shukrani nyingi kwa Asha Baraka kwa kufanikisha mpaka yeye kupata kiasi hicho cha fedha ikizingatiwa kwa sasa yeye kutokana na maradhi hawezi kufanya kazi kwa sasa.
𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗠𝗨𝗔𝗣𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗔𝗠𝗕𝗜 𝗞𝗨𝗪𝗔
𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗠𝗕𝗢 𝗬𝗔 𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂
𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 akimuapisha Mhe. 𝗣𝗮𝘁𝗿𝗼𝗯𝗮𝘀 𝗞𝗮𝘁𝗮𝗺𝗯𝗶 wa Mambo ya
Ndani...
1 minute ago
0 Comments