African Stars Entertainment imemchukua Mshindi wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis kwa ajili ya kunengua kwenye Bendi yake ya African Stars "Twanga Pepeta".
Mary Khamis amechukua nafasi ya mnenguaji Aisha Madinda aliyetimkia katika Bendi ya Extra Bongo. Mpaka kufikia hatua ya kumchukua Mary ni baada ya kuvutiwa na kiwango chake cha uchezaji kwa kuwa alionyesha kipaji cha hali ya juu cha uchezaji katika shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 na hatimaye kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano hilo lililoisha hivi karibuni hivyo Aset ina amini hapo baadae atakuwa mmoja wa madansa hodari hapa Tanzania.
Kwa sasa Twanga Pepeta ina wanenguaji wa kike tisa na wa kiume wanne, ambao ni Abdillahi Zungu, Kassim Mohammed au Super K, Bakari Kisongo au Mandela na said Mtyanga hao ni safu ya unenguaji wa kime na kwa wanawakie ni pamoja na Fasha Sunday, Beatrice Mwangosi au Baby Tall, Asha said au Asha Sharapova, Regina Filbert, Grace Kaswaga, Vicky Pandapanda, Lillian Tungaraza au Internet, Sabrina Mathew na Maria Soloma.
ASHA BARAKA.
MKURUGENZI ASET.
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
1 hour ago
0 Comments