Meneja Masoko wa Benki ya Exim Tanzania Linda Chiza(kushoto) akipeana mkono naRais wa Lions Club Tanzania Frank Goyayi wakati wa makabidhiano ya mfano wahundi ya milioni moja kutoka benki hiyo kuchangia matibabu ya wagonjwa wa machonchini.Katikati ni Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi na wa pili kushotoni Meneja Mkuu wa Benki ya Exim dinesh Arora na kulia ni Mkurugenzi wa benkihiyo Hanif Jaffer.

Baadhi ya Wanamitindo walioshiriki katika onyesho maalumu la mavazi la ‘Fashion4 Vision’ lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam maalumu kwa kuchangishafedha kwa ajili ya wagonjwa wa macho nchini ambapo sh. milioni 15/-zilipatikana. Onyesho hilo lililoandaliwa na Lions Club kwa pamoja na Wabunifuwa Mavazi Mustapha Hassanali na Jamila Veraswai na kudhaminiwa na Benki ya EximTanzania.
Na Mwandishi Wetu
ONYESHO maalumu la mavazi llinalobeba ujumbe wa ‘Fashion 4 Vision’lililofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam limechangisha sh. mil 15/-zitakazosaidia matibabu ya wagonjwa wa macho nchini.Onyesho hilo liliandaliwa na Lions Club Tanzania chini ya uratibu wa Wabunifu waMavazi Mustapha Hassanali na Jamila Veraswai na kudhaminiwa na Benki ya EximTanzania ambapo vitu mbalimbali yakiwemo mavazi ya mitindo tofauti yalinadiwa namgeni rasmi Mama Salma Kikwete kwa waliohudhuria.Akizungumzia onyesho hilo Mama Salma aliipongeza Lions Club pamoja na wabunifuHassanali na Veraswai kwa kuwa na mawazo chanya ya kusaidia jamii ya kitanzaniaambapo pia aliwashukuru na kuwapongeza wote waliojitokeza katika onyesho hilo nakuchangia kutunisha mfuko kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa husika.“Ni mawazo yanayopaswa kuungwa mkono na mimi binafsi nawapongeza Lions pamoja nawabunifu wetu kwa kuonyesha moyo wa imani kwa wenzetu wanaosumbuliwa na maradhilakini niwapongeze pia waliojitokeza leo na kuchangia fedha”,alisema MamaKikwete.Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Benki ya Exim Dinesh Arora alisema pamoja naudhamini wamechangia sh.milioni moja katika mfuko huo na kwamba hiyo ni katikautekelezaji wa majukumu ya kawaida ya kibenki kwa jamii ya kitanzaniawanaochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa benki hiyo.“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini piatumekuwa na majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini pamoja namchango wetu katika hafla ya leo ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo,”alisema Arora.Rais wa Lions Club Frank Goyayi alisema hafla hiyo ilitarajiwa kukusanya sh.milioni 10/= lakini ni jambo la kutia moyo kuona wamevuka lengo na kwamba hiyoinawahakikishia kuwa watafanikiwa katika yale waliyoyalenga kwa wagonjwa wamacho nchini.“Tumefarijika na kututia moyo kwa kiasi kikubwa na sasa tuna imani ya kufanikiwakatika yale tuliyoyalenga,tunawashukuru wote waliojitolea kudhamiani nakuchangia kwa moyo wao wa upendo kwa wenzao wanaosumbuliwa na maradhi,” alisemaGoyayi.

Post a Comment

0 Comments