TUDUMISHE USHIRIKIANO NA HAKI SAWA KATIKA KAZI NA JINSIA ZOTE.
KILIMO KWA KUTUMIA NGOMBE.
KUFANYA KAZI KWA NIDHAMU MAANA YAKE NI KUJITUMA MWENYEWE.
Hizi picha zimezunguka mnara huo hapo juu na bila shaka zina maana yake lakini zimeanza kuchakaa kiasi cha kuhofia kupotea kwa taswira hii yenye kumbukumbu muhimu katika taifa hili.
Picha ya juu ni mnara wa Azimio la Arusha ambao ndiyo unaitambulisha jiji la Arusha. Itambulike kuwa Azimio la Arusha lilikuwa na lengo la Ujamaa na Kujitegemea kama unavyoona hizo picha ambazo zimo pembeni kwa mnara huo.
Mnara huo wa Azimio la Arusha ulikuwa na madhumuni ya kuwafanya watambue kuwa:
(a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
b) Kwamba kila mtu anastahili heshima
(c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki yakushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, yaMikoa hadi Serikali Kuu;
(d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazoyake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka nawa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
(e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamiihifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwamujibu wa Sheria;
(f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya hakikutokana na kazi yake
(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asiliwanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamanakwa vizazi vyao;
(h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwendasawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njiamuhimu za kuukuza uchumi; na
(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ilikuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonyamtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kinginena kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatanina siasa ya watu wote kuwa sawa.
0 Comments