TFF WAFUNGUKA UMRI WA MCHEZAJI MRISHO NGASSA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa lengo la kukiimarisha kabla ya mechi ya marudiano ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon itakayofanyika Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa (Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar). Baada ya uamuzi huo wa kocha, baadhi ya washabiki na vyombo vya habari vimeonesha mashaka juu ya umri wa Ngasa. Kwanza TFF inapenda kuweka wazi kuwa umri chini ya miaka 23 ndiyo sifa ya msingi ya kuchezea timu hiyo. Hivyo uamuzi wa kocha kuita wachezaji hao mbali ya vigezo vingine, cha umri pia kimezingatiwa. Umri wa Ngasa aliyezaliwa Aprili 12, 1989 ni miaka 22. Wachezaji wengine walioongezwa na tarehe zao za kuzaliwa ni Makasi (Februari 2, 1990), Luhende (Januari 21, 1989), Aziz (Januari 1, 1989), Chale (Juni 19, 1992), Lundenga (Septemba 12, 1990) na Abdul (Novemba 10, 1992). Boniface Wambura Ofisa Habari

Post a Comment

0 Comments