Social Icons

Sunday, April 17, 2011

REHEMA JUMA PENZA NA AMRI KAMALA WAMEREMETA,BONGO DAR ES SALAAMBwana Harusi Amri Kamala akiwa na Maiwaifu wake Rehema Juma Penza ambao jana walifunga ndoa nyumbani kwao na Rehema Gongo la Mboto Dar es Salaam na kufuatiwa na hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Red Onion uliopo katika Jengo la Haiderry Plaza katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana usiku. Hapa ilikuwa ni wakati wa bwana na bibi harusi kufungua muziki.Rehema akimlisha mumewe Bwana Kamala kipande cha keki.Ikawa zamu ya Rehema kulishwa na mumewe Amri.

Hapa ni mpango mzima wa kukata keki ndani ya ukumbi wa R ed Onion uliopo katika jengo la Hiderry Plaza katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Pendo Penza akifurahi mara baada ya kucheers na maharusi hapa akiwa na mpambe Juliana Penza. Bwana Kamala akicheers na mai -wife wake Rehema Penza anayeshuhudia ni Mpambe wa Bi Harusi Juliana Penza. Na mimi mama Fetty Penza nilikuwepo hapa nikicheers na Bi Harusi wetu Rehema Penza. Bi Harusi Rehema Juma hapa akicheers na mdogo wake Fety Juma Penza.


Kutoka kushoto ni Kaka wa Bi Harusi Idd Penza, aliyekuwa DJ wa shughuli Seif Katunda na mimi niliyekuwa MC wa shughuli.

Kutoka kushoto ni Mrs. Rukia Mashaka Penza, Rehema Penza na Mama Fetty Penza. Mimi Kushoto na Bibi harusi Rehema Penza tukiwa katika picha ya ukumbusho.
Mimi na Baby Chancy wa Ukweli 'JP Junior' .Binafsi nachukua fursa hii kuwawakilisha famila ya Penza na wadau wengine kwa kuwapa pongezi Maharusi hawa na kuwatakia maisha mazuri yaliyojaa furaha, upendo na amani.Inshaallah Mwenyeezi Mungu Subhanahuwataala awajaalie kheir na baraka Amiin.

1 comment:

Unknown said...

Waaaaooooo. Hongera sana Rehema na shemeji yetu, kwa kufunga ndoa. Hata mwaliko jamani. Mie binafsi nawatakia maisha mema na yenye furaha kila siku. Mmmmhhhh wedding dress ni mwisho. Mbona nimepitwa jamani. MC, Fetty, Upendo na warembo wote shopping ni wapi jamani maana mlivyopendeza. Haya nimeikosa hiyo lakini angalau nimeambulia picture. Rehema kila la kheri.

 
 
Blogger Templates