Wakulima nchini wametakiwa kutumia eneo dogo na kuzalisha kwa tija wakiwa na uhakika wa soko.
"Sisi kwa upande wetu kama serikali tutahakikishs tunawapatia soko la uhakika" amesema Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo.
Amesema kuwa uzalishaji ambao unaongozwa nantaarifa sahihi lakini pia maarifa.
"Sisi kwa upande wa serikali chini ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan tutaendelea kuweka mazingira rafiki ya uzalishaji na kuwapunguzia gharama wakulima kwa kutengeneza barabara kwa kushirikiana na TARURA kwa kutengeneza barabara na madaraja ambazo zitafikika katika kipindi cha mwaka mzima kutoka kwenye mashamba kwenda kwenye masoko na kuwapunguzia gharama za pembejeo za kilimo " amesisitiza Londo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Denis Londo, amesema hayo tarehe 7 Agosti 2026 katika maonesho ya nanenane yanayofanyika katika Viwanja Dkt. John Samuel Malecela Jijini Dodoma ,amesemma kuwa nchi ya Tanzania inapaswa kutumia taarifa sahihi za masoko kama nyenzo muhimu ya kuongeza ushindani wa bidhaa zake katika masoko ya kikanda na kimataifa, badala ya kuzichukulia kama taarifa za kawaida.
Aidha amesema kuwa matumizi sahihi ya taarifa hizo yatasaidia kuharakisha mageuzi ya uchumi na kuimarisha biashara ya mazao ya kilimo nchini na hata nje ya nchi.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, katika hafla iliyoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Dodoma.
Wakati huohuo amesema kuwa hivi sasa dunia ya biashara inabadilika kwa kasi sana kutokana na mabadiliko ya mahitaji ya walaji, viwango vya ubora, matumizi ya teknolojia za kidijitali pamoja na kuzipima.mbegu kwa mashine bila ya kupoteza muda wa kwenda maabara kwa sababu kwa kutumia teknolojia majibu ni papo kwa papo na hivyo Tanzania haihqina budi kwenda sambamba na kasi hiyo.
Kwa mujibu wa Londo, utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2023 pamoja na programu mbalimbali za maendeleo ya kilimo unahitaji uzalishaji unaoongozwa na mahitaji halisi ya soko, badala ya kuzalisha kwanza na kutafuta wanunuzi baadaye.
Pia ametoa wito kwa taasisi zinazohusika na sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, mamlaka za udhibiti, taasisi za fedha, serikali za mitaa pamoja na sekta binafsi kushirikiana kuhakikisha taarifa za masoko zinawafikia wadau kwa wakati.
Amesema kuwa hatua hiyo itawawezesha wazalishaji na wafanyabiashara kufanya maamuzi sahihi kuhusu uzalishaji, uongezaji thamani na biashara ya mazao.
"Tanzania hayapaswi kupimwa kwa ongezeko la mauzo ya bidhaa nje ya nchi pekee, bali pia kwa kuongezeka kwa ajira, mapato ya wananchi na ukuaji wa viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao" amesema.
"Nafasi ya kijiografia ya Tanzania, inayopakana na nchi nane, inatoa fursa kubwa kwa nchi kuwa kitovu cha biashara ya mazao ya kilimo, endapo kutakuwa na uratibu mzuri wa uzalishaji, uongezaji thamani na biashara" amesema Londo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo kwa utaratibu wa Shoroba Tanzania (AGCOT), Geoffrey Kirenga, amesema matumizi ya sayansi na teknolojia yanaweza kusaidia Tanzania kufikia masoko mbalimbali duniani kwa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinakidhi viwango vinavyohitajika katika masoko hayo.


0 Comments