MECHI U23 VS CAMEROOM WAINGIZA SH. 31,681,000.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


MAPATO U23 v CAMEROON


Mechi ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya umri wa chini ya miaka 23 na Cameroon iliyofanyika Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 31,681,000.

Baada ya kuondoa sh. 4,832,694.92 ambayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), fedha iliyobaki kwa ajili ya mgawanyo ni sh. 26,848,305.08. Gharama za awali za mechi kabla ya mgawanyo zinazojumuisha kamishna na waamuzi, uchapaji tiketi, ulinzi, usafi wa uwanja, umeme na kampuni ya Beijing Construction ya China ni sh. 17,458,000.


Mgawanyo wa mapato baada ya kuondoa gharama za awali ni sh. 939,030.51 ambayo ni asilimia 10 ya gharama za mchezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 469,515.25, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 7,042,728.81 na asilimia 10 ya uwanja ni sh. 939,030.51. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP A, sh. 5,000 kwa VIP B na VIP C wakati viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa ilikuwa sh. 1,000.


MPINZANI WA U23

Timu itakayocheza na U23 katika raundi ya pili ya michuano ya mchujo ya Olimpiki itajulikana Aprili 13 mwaka huu wakati shughuli ya upangaji ratiba itakapofanyika makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.


U23 ni moja ya timu 16 zilizofuzu kwa ajili ya raundi ya pili ambayo mechi za kwanza zitachezwa kati ya Juni 3, 4 na 5 na zile za marudiano kufanyika kati ya Juni 17, 18 na 19 mwaka huu.


Afrika katika michezo hiyo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London, Uingereza itawakilishwa na timu tatu. Nafasi ya nne itagombewa na timu za Afrika na Asia zilizoshika nafasi ya nne katika mchujo katika kwenye mabara yao.

Timu hizo zitacheza mechi hiyo (playoff)

Aprili 12 mwakani jijini London.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Post a Comment

0 Comments