Wakuu,
Napenda kutoa ushuhuda wangu katika mjadala wa Loliondo ambao umekuwa ukivuma sana katika blog zetu kwa siku za hivi karibuni. Hongera sana kwa vijana wetu wakina, Generali ulimwengu, Magidd Mjengwa, mashaka john na bwana Juma Mwilima. Hawa vijana wameongea mengi sana ya maana, na ninaungana nao katika hili, kwani hakuna cha tiba wala cha nini kwa babu. Wale wote waliojifanya wamepona, ndo wale wanaokufa. Kwanza, mimi ni Muhathirika wa Ukimwi. Niliomba ruksa ya dharura ofisini, nikafungasha, na kuondoka kwenda kwa babu. Nilipata kikombe changu baada ya siku nne tu. Kwa sasa nadhani inachukua zaidi ya wiki au mbili kumfikia babu. Yalioyonikuta Loliondo, naogopa hata kuadisia; tulilala nje kwa kipindi chote. Nilishudia watu waliokuja na dripu toka hospitalini. Kweli watu wamekata tamaa humu nchini. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV’s nikiamini nimepona kwani nilikuwa nazani nimepona , ghafla hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Nilizirudia ARV zangu na sasa hali yangu imeanza kuimarika kiasi Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, karudi, na kuanza kutangaza kwamba kapona. Jana (jumapili) hali yake ikawa mbaya kweli, ikabidi tumpeleke hospitali ya Amana ambako amelazwa hadi sasa hivi. Ina maana wiki tatu aliamini amepona, kumbe ugonjwa ukawa unamtafuna zaidi. Nadiriki kusema wazi kwamba sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu, kama yupo ajitokeze na kutoa ushuhuda wake wa ukweri. Kilichonishangaza zaidi ni hali niliyoikuta loliondo. Nikiwa kwenye foleni, watu wanne wamefariki pale nikiwatazama, ila kuna mdada wa makamu alikata roho akisubiri muda wake wa kupata kikombe. Cha ajabu, ndugu zake badala ya kuurudisha mwili wake kwao Dodoma, walijifanya kuondoka naye na matokeo yake kumtupa njiani kama kilometa 20 toka hapo kwa babu. Watu wengi wametupwa njiani, hasa pale ndugu wanaposhindwa na cha kufanya. Ili kuiokoa jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko huko loliondo na watu kutupwa kama wanyama polini, serikali inabidi iingilie kati, kwani hali ya loliondo ni mbaya zaidi na viombo vya habari vinatufichia ukweli…jamani, kuna kitu loliondo, kuna kitu kinafichwa. aliyepima kabla ya kwenda loliondo na kuonekana na vilusi, na kupata matokeo negative baada ya kutoka loliondo, ajitokeze. Mimi sikuluka foleni, na nilikuwa na imani kubwa sana kwamba nilipona , mpaka hali yangu inakuwa mbaya nilidhania nimepona.
Chanzo www.burudan.blogspot.com
1 Comments
Tunaomba waje wajitokeze, watuambie, kuwa walikua wanaumwa na vyeti vya kuumwa hivi, na baada ya kikombe wakaenda tena kupimwa na vyeti wakapewa tena na tuvione!
Zaidi ya hapo itakua kudanganyana tu kama kawaida yetu.
Mara popo bawa, mara babu Loliondo, mama Tabora, Mama Morogoro, sijui ukiua albino unakua tajiri, au kuiona bibi kizee mwanza au shinyanga basi mchawi, au “wataalam” wamejaa Bagamoyo! Au Sumbawanga kumejaa wachawi na waganga (wakati ni maskini wa kutupwa, huku rasilimali za kila aina zimezagaa tu!).
Tuachane hayo mambo ya imani za ajabu.
Tukumbuke dini ilianzishwa na binadamu na ndo maana kila kukicha wazungu wanabadilisha masharti ili yaendane na maisha yao! Kama waarabu ndo usiseme, yalioandikwa kwenye koran yanakua machungu kwao, wanataka “democracy” isio na “majahedinas!”
Leo sisi ndo tunajifanya hzio dini tulianzisha sisi na tuanzijua kinoma!
Fumbueni macho wabongo!