YALIYOJIRI MWISHO WA WIKI CINE CLUB, BONAZA LA WANAHABARI LAFANA

Imelda Mtema(Global Publishers),Khadija Kalili na Dina(Free Media) ilibidi nibonyee kutokana na urefu niweze kuonekana vizuri na Asha Baraka Mkurugenzi ASET tukiwa Cine Club, Mikocheni katika Bonanza la wanahabari . Mdau nambari Moko mtembelee katika www.mtaa kwa mtaa.blogspot .com ili upate mambo yake.
Mwandishi wa Mwananchi Clara kushoto akimkaribisha Mkurugenzi wa Redio Uhuru Mikidadi Mahmoud.
Dina Ismail(Tanzania Daima-www.Mamapipiro.blogspot.com), Mussa Mateja katikati (Global) na Rose Mama Jeniffer ambaye ni Star kwenye filamu ya Anco JJ.
Baadhi ya Wahariri wa Habari kabla kuanza mbio.
Kambi Mbwana kutoka New Habari akionyesha umahiri wake katika muziki. wa vyombo vya habari nchini mwishoni mwa wiki waliweza kukutana jijini Dar es Salaam, kwenye fukwe za Cine Club huku wakifurahia pamoja ikiwemo kucheza michezo mbalimbali katika Bonanza maalum kwa ajili ya kufahamiana na kubadilishana mawazo maarufu ‘Media Day’ lililoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) nakudhaminiwa na Kampuni ya bia Tanzania (TBL).
*************************
Katika Bonanza hilo waandishi waliweza kucheza michezo kadhaa, ikiwemo mpira wa miguu,wavu,pete,riadha, kuvuta kamba, mashindo ya kucheza dansi na mingine mingi ilikuwa imetia fora kwa waandishi pale walipoonyesha viwango vyao kwenye michezo hiyo huku Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa mgeni rasmi.
Ni hakika katika Bonanza hilo ambalo hufanyika kila mwaka limeweza kuwa chachu kwa kuendeleza michezo na kuimalisha afya kwa waandishi, Mara zote waandishi wamekuwa wakitumia fani yao kuelezea michezo hiyo hivyo kwa kufanyika bonanza maalum ni uwezo tosha ambao utasaidia kwa wao kuwa na uwezo wa kujituma katika kufanya mazoezi ilikujiweka fiti.
Kwa kiasi kikubwa malengo ya waandishi wahabari yamefanikiwa kutokana na kuwepo na ushirikiano mzuri kataka kulifanikisha pamoja sambamba na mwitikio mzuri wa watu ikiwemo utulivu wakutosha na utaratibu mzuri katika kulifanikisha hili ikiwemo kufanyika kwa amani kwani kila timu ilicheza kwa uwezo wake sambamba na kujiamini hali hiyo ilipelekea bonanza hilo kufanyika kwa utulivu mkubwa.
Bonaza hili ni mara ya pili kwa TASWA na TBL kuandaa katika kuwakutanisha waandishi kuungana pamoja katika kufahamiana kupitia michezo mbalimbali ambapo vyombo vyote vinashiriki katika michezo yote, Kwa nyakati tofauti viongozi wa TASWA, wanasema kuwa Bonanza hilo ni chachu kubwa kwa chama hicho kwani linasaidia kuongeza chachu ya kuwaweka na kuwakutanisha karibu wadau mbalimbali wa fani ya habari.
“Ni hakika Bonanza hili ni chachu katika kuendeleza umoja wetu sisi wanahabari pasipokuangalia ubaguzi wowote kila mmoja wetu anahaki sawa na mwengine ndio maana wanahabari wote leo wameweza kushiriki” anasema Katibu msaidi wa Taswa, Amiri Mhando.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani Juma Pinto anasema waandishi kukutana katika siku moja kwa mwaka ni historia ambayo haitaweza kusahaulika miongoni mwa waandishi chipukizi na wakongwe .
Akielezea juu ya tukio hilo Machi 12, Pinto anasema TASWA imedhamiria juu ya waandishi kuwa na taratibu za kupata kujuana katika michezo zaidi kutokana na kuwa na majukumu yao ambayo kila siku wanashindwa kuyatatua hivyo Bonanza hilo linaweka siku ya kukutana na kupata kucheza michezo hiyo na kuburudika
Pia alisema kuwa kwa sasa waandishi wanachangamoto nyingi ambazo zinahitaji kupata ufumbuzi katika kazi zao hivyo kuwa na bonaza nisehemu pia ya kuweza kujadili changamoto zinazo wakabili ndani ya tasnia ya habari kiujumla.
“Mimi naamini kupitia bonaza tutakuwa tumejifunza mengi katika fani yatu pamoja na kuonana na wengine ambao hawaonekani mitaani kutokana na kuelemewa na majukumu makubwa pia TBL imeweza kuwaleta pamoja “.anasema Pinto
Pinto anasema kuwa waandishi wa habari ni watu muhimu ambao wanahitaji kusaidiwa na kuwafanya nao kuwa miongoni mwanaotambauliwa katika michango yao hata kuonana kwao inakuwa furaha zaidi .
“Kwa kiasi kikubwa malengo ya waandishi wahabari yamefanikiwa kutokana nakuwepo na ushirikiano mzuri kataka kulifanikisha pamoja na kuwepona mwitikio mzuriwa watu ikiwemo utulivu wakutosha na utaratibu mzuri katika kulifanikisha hili pamoja na kuwanaushirikiano mzuri katika kilajambo “.anasema Pinto.
Hatahivyo alisema waandishi waendelee katika kuwa na moyo huohuo ilikuweza kuwafanya waweze kufikia mbali kimichezo na sehemu nyingine ili kuwasaidia watu wengine waweze kuiga kutoka kwao .
Michezo ilichezwa kwenye Bonanza hilo ni soka ya ufukweni (wanaume), netiboli (wanawake), wavu (jinsia zote walichanganyika), mbio za magunia (wanawake na wanaume), mbio meta 100, kuruka kichura (wanawake na wanaume) na kuvuta kamba (jinsia zote walicheza) na kucheza muziki (wanawake na wanaume).
Kiongozi wa Twanga Luizer Mbutu na Janet Isinika muimbaji.
Mpiga ngoma wa Twanga Kaboshoo.
Asha Baraka akishangaa mtindo wa nywele za Msanii Joti ambapo ameweka staili ya Antena, huku akiwa amesokota vifungu viwili tu.
Watu na Kazi zao bwana Mzee wa Chiajie Ahmad Issa Michuzi wa http://www.jiachie/ Blogspot.com ,akiwajibika.
Dogo Rama Muimbaji anayekuja juu katika bendi ya Twanga.
Ben Kinyaia naye alikuwepo.
Janet Isinika pambo la Twanga akiwa jukwaani.
Isakwisa Mwaifuge yeye aliachia pozi hili.

Asha Baraka akisalimiana na aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye Bonanza hilo Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi .
Mazungumzo yalikuwa hayaishiiiii.
Wahariri wa kike kutoka kushoto ni Angel Akilimali wa Redio Uhuru, Jane Mihanji Mhariri wa Gazeti la Uhuru na Grace Hoka Mhariri wa Michezo Gazeti la Bingwa.Hapa kabla hawajashiriki katika mbio za mita fupi ambapo walishindwa vibaya.
Bongowekeend nikijivinjarii.
Dina Kushoto na Clara Alphonce kutoka Mwananchi.
Ilikuwa ni kufurahi kwa kwenda mbele yaani hapa hata sikumbuki nilifurahishwa na kitu gani aliyenyanyua mikono ni Eliza Mayemba na bonge White ni Mwani Nyangassa wa The African.
Somoe Ng'itu (Nipashe) , Juti Kumbi wa gazeti la Sani na Mimi tukijiachia kwa raha zetu.
Charlz Baba akiwa na wasanii wa Twanga.

Post a Comment

0 Comments