*************
Ramadhani Kassim (33)ambaye ni mkazi wa Wazo Jijini Dar es Salaam jana ametangazwa kuibuka kidedea mara baada ya kushinda droo ya Tigo na kunyakua gari aina ya Nissan Hardboy.
Mshindi huyo ambaye ni dereva wa gari la kubebea mchanga alipigiwa simu akiwa katika eneo lake la kazi na kila alipoulizwa endapo angeshinda alipenda zawadi gani yeye alionekana kumwachia mungu na kusema chochote atakachopata atafurahia.
Kassim ambaye alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kupigiwa simu amesema amefurahi kwa sababu amekuwa akishiriki droo nyingi za Tigo.
Droo hiyo ambayo ilichezeshwa jana katika Makao Makuu ya Tigo Jijini iliweza kupata washindi wengine ambao wameshinda fedha taslimu.
Washindi hao ni pamoja na Janet Hohn mkazi wa Ubungo ,aliyeshinda kitita cha Milioni mbili, Alfa Temba sh.mil1., Isack Elius sh. Mil.1 mkazi wa Ukonga , Wakili Zefania Msuya ambaye ni mkazi wa Vingunguti ameshinda kitita cha Mil.1 na Ignas Jacob mkazi wa Arusha ambaye yupo jijini kwa matibabu amepata sh. 500,000.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Habari wa Tigo Jackson Mbando ametoa wito wadau kuendelea kucheza bila kukata tamaa.
Mbando alisema droonyingine ya gari imepangwa kuchezeshwa Machi 28 mwaka huu.

0 Comments