Kutoka Kushoto ni Ofisa Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Bahati Singh, Mkurugenzi wa Mahusiano SBL ,Teddy Hollo Mapumba na Ofisa wa Mambo ya Ndani SBL Imani Lwinga wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo.
Dar Es Salaam, 14 March 2011: Diageo, kampuni kubwa ya biashara ya vinywaji duniani, leo inatangaza majaji wanane kwa ajili ya tuzo za Diageo Africa Business Reporting Awards zitakazotangazwa rasmi tarehe 30 Juni 2011. Tuzo hizi za mwaka zilizindiliwa mwaka 2004, kwa ajili ya kuwapa hamasa waandishi wa habari kuripoti habari fursa za kiuchumi barani Afrika na kusherehekea uandishi bora wa habari za biashara.
Mwaka huu tunashuhudia kurejea kwa majaji kadhaa mahili kutoka vyombo kadhaa vya habari, sekta ya biashara, serikali na taasisi za maendeleo. Jopo la majaji la mwaka huu linahusisha wafuatao.
Shantayanan Devarajan ni mchumi mkuu wa Benki ya Dunia, Kitengo cha Afrika na anashughulika na “Afrika Inaweza” blog inayosomwa sana ikijihusisha na habari motomoto zinazohusu habari za maendeleo ya kijamii na uchumi barani Afrika. Amefundisha vyuo vikuu vya biashara duniani akihamasisha ukuaji wa sekta binafsi katika Afrika.
Zeinab Badawi ni mtangazaji mahili wa habari wa kimataifa na msomaji wa habari wa BBC World News Today na pia mmoja wa wadhamini wa BBC World Service Trust.
Baroness Shriti Vadera ni waziri wa zamani serikalini katika wizara ya maendeleo ya bishara, ubunifu na ufundi. Baroness Vadera alikuwa pia waziri katika wizara ya maendeleo ya kimataifa na mjumbe katika baraza la ushauri wa masuala ya uchumi – hazina pamoja na kuwa mshauri maalumu wa waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown. Desemba 2010 aliteuliwa kuwa mjumbe wa boadi ya BHP Billiton na AstraZeneca kama mkurugenzi.
Stephen King ni mtaalamu wa uwekezaji The Omidyar Foundation. Kabla ya hapo alikuwa mkurugezni wa BBC World Service Trust na alifanya kazi zaidi ya miaka 15 katika shirika la maendeleo la kimatiafa katika nchi za Asia, Afrika na Amerika Kaskazini
.
Dr Alhaji Bamanga Tukur ni Mwenyekiti wa NEPAD Business Group. Pia ni mwenyekiti wa BHI Holdings Limited na Rais wa African Business Roundtable.
Louis Michel ni Kamishina wa zamani wa shirika la maendeleo na misaada la Ulaya. Kabla ya hapo, alikuwa ni mmoja wa watu wa juu katika serikali ya Ubelgiji ambako alikuwa waziri wa mabo ya nje, waziri katika wizara ya uboreshaji wa taasisi na naibu waziri mkuu.
Professor Wiseman Nkuhlu ni Mtendaji mkuu wa New Partnership for Africa’s Development (NEPAD). Kwa sasa ni mwenyekiti wa Pan-African Capital Holdings (Pty) Ltd, na mkurugenzi wa Old Mutual PLC, Kagiso Trust Investment na Virgin Atlantic South Africa.
Jopo la majaji litakuwa chini ya mwenyekiti ambaye ni mtendaji mkuu wa Diageo Bw. Paul Walsh. Jopo litachagua washindi katika tuzo zote 11.
Teddy Mapunda
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kampuni
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
4 hours ago
0 Comments