TAHADHARI WAPENDA MISHIKAKI MTALISHWA NYAMA YA PAKA

Wadau hasa wale wapenda mishikaki ile ya barabarani siyo hii ambayo hapa tulikuwa tukijisevia katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Dar es Salaam.Kuna jamaa anauza nyama za PAKA anawakama na kuwachinja mwenyewe kicha anachuna ngozi na kuuza. Mwenyewe anadai kwamba PAKA wa maeneo ya Upanga wamenona sasa sijui ni wale wanaoshiba bila kutozwa kodi MUHIMBILI au ni vipi.Jamaa huyo muuza nyama za PAKA alihojiwa hivi karibuni katika kituo cha Redio 88.4 Clouds FM na kukiri kuwa yeye anauza na mishikaki yake hailali.Kwa siku anauza nyama za Paka kati ya wanne hadi sita.Tena akajisifu anatia vikorombwezo vyote muhimu haya walaji kazi kwenu kwani hakutaja jina wala mahali anapofanya biashara hiyo.TAHADHARI KULAKULA HOVYO UNAKULA VIMISHIKAKI VYA PAKA.Mwenyewe anadai anasomesha watoto na kulipa kodi ya pango la nyumba kwa biashara hiyo Hii ndiyo Bongo Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments