Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Jan Poulsen akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini,( TFF) wakati wa kutangaza kikosi cha wachezaji wataocheza na timu ya Jamhuri ya Kati katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012 zitakazofanyika Ikweta ya Guinea na Gagon. Kulia ni Ofisa Habari wa Shirkisho hilo, Boniface Wambura na kushoto ni mwakilishi wa wadhamini, kutoka Kampuni ya Serengeti Meneja wa Bia ya Premier Serengeti Lager, Allan Chonjo.
Na Mwandishi Wetu
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya soka Tanzania, ‘Taifa Stars’ Mdenish Jan Poulsen jana alianika silaha zake 23 zitakazotumika dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mechi ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (CAN), inayotarajiwa kuchezwa Machi 26 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwarejesha kundini kipa Shaban Dihile na kiungo Mwinyi Kazimoto wa JKT Ruvu.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen alisema kikosi chake kitaanza kambi kesho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, ambao ameupa umuhimu wa hali ya juu ili afanikishe kufuzu kwa fainali hizo zitakazopigwa mwakani nchini Ikweta ya Guinea na Gabon.
Poulsen alisema, kwa sasa Tanzania iko nafasi ya tatu kandi kundi la nne, ikiwa na pointi moja, ikitanguliwa na vinara Afrika ya Kati na Morocco zenye pointi nne kila moja, wakati Algeria inayoshikilia nafasi ya nne ikiwa pointi sawa na Tanzania.
Aidha, Poulsen alisema, wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo, kwani inawezekana kutokana na ubora wa wachezaji wa Tanzania.
Mbali na kuwarejesha kundini maafande hao wa JKT Ruvu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwamo Stars enzi za Mbrazil, Marcio Maximo, pia amewaita nyota kadhaa wanaokipiga nje ya nchi, akiwamo Athuman Machuppa, Nizar Khalfan, Abdi Kassim ‘Babi’, Danny Mrwanda na Henry Joseph.
Kikosi kamili ni makipa Shaban Kado (Mtibwa), Juma Kaseja (Simba), na Dihile (JKT), wakati mabeki yuko Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Stephano Mwasika (Yanga), Haruna Shamte, Juma Nyoso na Kelvin Yondani (Simba), na Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya).
Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shaban Nditi (Mtibwa), Jabir Aziz (Azam), Henry Joseph (Kongsvinger IL Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu), huku washambuliaji ni Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver WhiteCaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mohamed Banka (Simba), Athumani Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam), na Mbwana Samatta (Simba).
DART yatoa safari nne za bure kwa wataonunua kadi
-
Na Mwandishi Wetu
Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imesema kuwa katika msimu wa siku
kuu za mwisho wa mwaka wanatoa sh.30000 kwa safari Nne kwa wa...
2 hours ago
0 Comments