MAVETERANI WA SIMBA vs YANGA KURUDIANA IDODOMYA

Wachezaji wa zamani wa klabu kongwe za Simba na Yanga, Madaraka Selemani, na Tom Kipese wote waliwahi kuchezea timu ya Simba wakiwa na Mratibu wa mechi hiyo Suleimani Mathew ambaye pia alicheza katika timu za Simba na Yanga katika nyakati tofauti pichani wakizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) wanatarajia kucheza mechi ya marudiano Aprili 23 mwaka huu, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Timu hizo ambazo ni watani wa jadi kutokana na zinapokutana kukamiana, zinatarajiwa kucheza mechi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kuvaana Machi 19 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini na Simba kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 likiwekwa kimiani na Shekhan Rashidi.

Mathew amesema mechi yao waliyocheza Jumamosi iliyoipita wameingiza kiasi cha shilingi Milioni 13 huku kiasi cha sh. milioni 1. Itapelekwa kwa wahanga wa Gongo la Mboto

Post a Comment

0 Comments