HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA INJILI WAIVA

Kampuni ya Tanzania Gospel Music Award Promoters imesema imeandaa tuzo za muziki wa Injili kwa lengo la kuhakikisha muziki huo unazidi kukua na kuhifadhiwa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shughuli hiyo, Harris Kapiga, katikati Mdhamini wa Tuzo kutoka mradi wa Zinduka Aunt Sadaka kushoto na Ofisa Masoko kutoka THT ,Michael Nkya. Kapiga alisema kuwa mchakato wa kupata wasanii watakaoshiriki tuzo hizo ulifanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi.
Alisema, shughuli ya utoaji tuzo hizo inatarajia kufanyika Machi 13 katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa wasanii zaidi ya 68 waliotengwa katika makundi tofauti.
Alisema, makundi hayo yalitokana na kupendekezwa kwa kupigiwa kura nyingi, ikiwemo tuzo za msanii bora wa kiume na kike kwa ujumla wa mwa mwaka, kundi bora, kwaya bora inayotumia vyombo vyote, isiyotumia vyombo na ile ya piano, mtayarishaji bora wa muziki na video.
Makundi mengine ni Bendi bora ya injili, Singo bora ya msanii wa kike na kiume, msanii bora wa kike na kiume, wimbo bora, wimbo bora toka nje ya nchi, video bora ya mwaka, mtunzi bora na balozi bora wa jamii.
“Muziki wa injili si wa kushindanisha, bali tunafanya hivyo ili kuhakikisha Watanzania wanamtukuza Mungu, pamoja na kuwatia moyo wasanii wa muziki huo ili waendelee kuhifadhi maandiko ya Injili,” alisema.
Upendo Kilahiro.

Shusho
Rose Mhando
Mwaitege.

Jen Misso.
Wanamuziki watano wa muziki wa injili wamebahatika kuingia katika kategori zaidi ya moja ya kuwania tuzo ya muziki wa injili TANZANIA.
Mratibu wa tuzo hizo, HARRIS KAPIGA amezitaja jumla ya kategori KUMI na NANE zitawaniwa katika shindano hilo.
Wanamuziki waliofanikiwa kuingia katika zaidi ya kategori zaidi ya moja ni JACKSON BENT JOHN LISSU , AMBWENE MWASONGWE , AARON KYARA , ROSE MHANDO , UPENDO NKONE BAHATI BUKUKU na CHRISTINA SHUSHO.
MSANII BORA WA KIUME KWA UJUMLA WA MWAKA .
JACKSON BENT
BONIFACE MWAITEGE
FANUEL SEDEKIA
AMBWNE MWASONGWE
JOHN LISSU.
MSANII BORA WA KIKE KWA UJUMLA WA MWAKA .
CHRISTINA SHUSHO
UPENDO NKONE
ROSE MHANDO
BAHATI BUKUKU
JANE MISO
UPENDO KILAHIRO.
KUNDI BORA LA MWAKA
UPENDO GROUP
THE VOICE
CANAN BROTHERS
TM MUSIC

Post a Comment

0 Comments