Kamati ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ( BD), imewapiga faini na kuwafungia wachezaji watatu wa timu za Savio na Vijana kutokana na kusababisha fujo zilizofanya mchezo huo uliopigwa Machi 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa kuvunjika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Ufundi BD, Manase Zablon, alisema kikao cha kamati hiyo kilichoketi juzi jijini, kimewafungia kifungo cha miezi sita na faini ya sh 200,000 kila mmoja, wachezaji Jije Makani wa Savio na Mohamed Ally ‘Dibo’ wa Vijana kutokana na kuzitwanga uwanjani jambo lililosababisha vurugu kuibuka kwa wachezaji wengine hadi kwa mashabiki pia, hivyo pambano kuvunjika. Alisema, pia Kamati hiyo imemfungia Herny Mwinuka almaarufu kama Kidume, wa Savio, kifungo cha mwaka mmoja kwa kuhusika na vurugu hizo na kumlima faini ya sh 300,000.
Kidume ni mchezaji mkongwe hapa nchini, ambaye alitoa mchango mkubwa ikiwamo kumnoa nyota wa Tanzania anayekipiga Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani, (NBA), Hasheem Thabeet, wakati huo akichezea UDSM Outsiders iliyokuwa chini ya Kidume.
Wachezaji hao wote, hawataruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote za mchezo wa kikapu hadi adhabu zao zitakapomalizika.
Mchezo baina ya timu hizo, ulivunjika kutokana na vurugu hizo zilizosababishwa na wachezaji hao zikiwa zimebaki sekunde 29 kumalizika, huku Savio wakiongoza kwa pointi 79-76.
Aidha, Manase alitoa onyo kwa wachezaji na viongozi ambao watajihusisha na vurugu zozote, watachukuliwa hatua kali ili kujenga nidhamu katika mchezo huo.
WATU WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MADAI YA KUHARIBU,KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA
RELI YA KISASA (SGR)
-
WATUHUMIWA Watano Wakiwemo Raia Wa China Wawili Wanaokabiliwa na Tuhuma
za Kuharibu Miundombinu Ya Reli Ya Kisasa (SGR) Wamepandishwa Kwa Mara
ya p...
2 hours ago
0 Comments