Na Dixon Busagaga, Moshi
ZAIDI ya wachezaji 100 wa gofu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani ya Kenya wanatarajiwa kukutana katika mashindano yatakayoshirikisha wachezaji wa kulipwa na chipukizi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo, ilieleza kuwa, michezo hiyo itafanyika katika uwanja wa gofu uliopo katika kiwanda cha sukari cha TPC mjini hapa kwa siku tatu mfululizo.
Ofisa michezo wa TPC, Peter Magera alisema, mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya uuzaji wa magari na mashine za mashambani ya Hughes Motors iliyopo eneo la USA River mkoani Arusha, yataanza Machi 18 hadi 20 kwenye viwanja hivyo.
Magera alisema, baadhi ya wachezaji watakaoshiriki ni wale wenye miaka zaidi ya 50, wa kulipwa pamoja na chipukizi, lengo kuu likiwa ni kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi.
“Katika mwendelezo wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Gofu Tanzania, mashindano haya yamelenga kuibua vipaji vipya, lakini pia kuwaenzi wachezaji wakongwe wa mchezo huu,” alisema Magera.
Alisema, zawadi katika mashindano hayo zimegawanyika katika makundi makuu matatu, zikiwamo za wanawake, wachezaji mahiri, chipukizi na nyingine ni kwa wale wenye miaka zaidi ya 50.
Ingawa alibainisha kuwa ni mapema mno kutaja aina ya zawadi, ofisa michezo huyo alisema, mchezaji mwenye umri mdogo, mkubwa, wanawake, chipukizi, wachezaji wenye miaka zaidi ya 50 na wale wanaopiga nyingi wote watapewa zawadi.
Aliongeza kuwa, lengo jingine la mchezo huo ni kuwaongezea pointi wachezaji mahiri katika mchakato wa kutafuta mchezaji bora kwa mwaka.
VIKAO KUANDAA MKUTANO WA 46 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC VYAANZA JIJINI
ARUSHA
-
Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
Ngazi ya Wataalam umeanza jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano huo
utakaof...
27 minutes ago
0 Comments