Na Dina Ismail
SIKU moja kabla ya kucheza mechi yake ya marudio dhidi ya Dedebit ya Ethiopia, Yanga imekiona cha moto baada ya kuwasili nchini humo tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa kesho kwenye dimba la Addis nchini humo. Akizungumza kutoka Ethiopia jana, msemaji wa Yanga Louis Sendeu alisema kwamba mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege walijikuta wakiganda kwa zaidi ya masaa manne kutokana na wenyeji wao kutofika na kuwapeleka katika hoteli. Alisema walifika saa 12:3o alfajiri ya jana lakini cha kushangaza walikaa uwanjani hapo mpaka kwenye saa 4:30 asubuhi ndipo walipokuja wawakilishi wa timu hiyo na kuwapeleka katika hoteli. Kama hiyo haitoshi Sendeu alisema hata hoteli waliyopelekwa iitwayo Ras ilikuwa haina sifa zinazostahili lakini pamoja na kulalamika wenyeji weao hao waliwaeleza kwamba haitowezekana kuwatafutia mahala pengine kwani timu zote huwa zinafikishiwa hoteli hiyo. SEndeu aliongeza kuwa hali hiyo, ilimfanya balozi mdogo wa Tanzania nchini humo Vicent Kibwana kuingilia kati na kuongea na wachezaji hivyo kulimaliza tatizo hilo.“Balozi alitueleza kuwa hali ile ni njama za kutaka kutuvunja moyo ili tufanye vibaya katika mechi yetu…tulirudisha mioyo nyuma na kuendelea kukaa hotelini hapo”, Alisema Sendeu.
Sendeo aliongeza kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri na jana jioni walifanya mazoezi katika uwanja watakaochezea.Yanga iliondoka usiku wa kuamkia jana huku kocha wake mkuu Sam akiwa na matumaini ya kikosi chake kurejea na ushindi wa mechi yake hiyo ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika (CAF). Akizungumza juzi, Timbe alisema katika siku chache alizokuwa na timu hiyo amezitumia kurekebisha mapungufu aliyoyaona tangu ambayo anaamini yatasaidia kushinda mechi hiyo. Alisema matumaini ya timu yake kushinda yanatokana na kiwango walichonacho wachezaji wake akilinganisha na wapinzani wao baada ya kuwaona katika mechi yao ya awali iliyopigwa nchini wiki iliyopita.“Niliiona mechi ya awali kabla sijajiunga na Yanga hivyo mapungufu ya timu yangu nimeyafanyia kazi nay ale ya waopinzani wetu pia tumeyafanyia kazi nadhani vijana hawataniangusha siku hiyo”, Alisema Timbe.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
5 hours ago
0 Comments