Na Mwandishi Wetu
WANACHAMA wa Yanga tawi la Tandale kwa Mtogole Jijini Dar es Salaam, wamesema chanzo cha migogoro inayoendelea hivi sasa ndani ya Klabu hiyo ni mfadhili wao Yusuph Manji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya wanachama wa tawi hilo Waziri Jitu mwenye kadi namba 001732 alisema, Manji amewagawa viongozi wa Yanga hali ambayo imesababishwa kuwa Yanga ya makundi makundi. Jitu alisema Manji amekuwa akijipandikizia vyeo, kwamba yeye ni mfadhili wao Mkuu wa Klabu hiyo bila kuthitishwa na wanachama, huku akibeba jukumu la viongozi na wanachama takribani 800 wenye haki ya kumteua Francis Kifukwe na kumpendekeza Mbunge wa Wilaya ya Temeke Abbas Mtemvu kuwa mdhamini huku akijitetea kuwa timu haina wabunge. Alisema Manji amekua na tabia ya kukataa viongozi ambako awali alimkataa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Klabu hiyo Iman Madega , na baada ya uchaguzi kufanyika wanachama walichagua viongozi wanaowataka ambapo alipanga majukumu kwa viongozi hao ndani ya siku 60 ya uongozi huo.Kama hiyo haitoshi Mfadhili huyo alitangaza kuwakataa baadhi ya viongozi akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Yanga Devis Mosha.“Manji amejijengea desturi ya kutuchagulia viongozi anaowataka yeye na kuwakataa viongozi tuliowachagua sisi kwa kuona wanaweza kuifikisha mbali Klabu hii na kuchagua viongozi anaowataka yeye kwa maslahi yake binafsi,“Yusuph Manji kwa sasa siyo mfadhili wetu tena wa Yanga bali ni mfadhiliwa wa Yanga , yeye amebaki kuwa mkopeshaji mkuu wa Yanga na tunataka kuwaambia kwamba wale viongozi tuliowachagua tukiwa na akili timamu hivyo awaache wafanye kazi zao inavyotakiwa“ alisema Jitu.Alisema Manji alisaini mkataba wa kuifadili Klabu hiyo kwa muda wa Mwaka mmoja ambao alisaini wakati wa uongozi wa Madega, ulishamalizika ambako alimtaka kusaini tena upya kwakuwa mlango upo wazi na siyo kufanya mambo kinyume na taratibu za Klabu hiyo kupitia mlango wa nyuma.Jitu alisema ktokana na jinsi hali ilivyo sasa kila kiongozi unaye muuliza kinachoendelea hajui ikiwapo Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo hali ambayo inaendeleza mitafaruku na wanachama hawajui cha kufanya zaidi ya kumtaka Manji aondoke haraka iwezekanavyo Yanga kwa sababu ndiyo anayetumia pesa zake kuleta migogoro hali ambayo wamechoshwa nayo.Naye mwanachama Juma Kassu mwenye kadi namba 006876, alisema awali Manji alimlazimisha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Iman Madega kwamba anataka kuwa mmiliki mkuu wa Klabu hiyo jambo ambalo lilipingwa, lakini bado alitumia mgongo wa ufadhili Yanga.Aidha,Kassu alisema kuwa kuondoka kwa Kaimu Katibu mkuu wa Klabu hiyo kuna mashaka sana kwa sababu alitangaza kuumwa halafu ameajirwa kwenye Kampuni ya Quality Group ambayo mmiliki wake ni Manji huku kazi na maamuzi ya Yanga mengine yanafanyika kwenye Kampuni hiyo wakati Yanga ina Ofisi zake.Alisema wao wanachojua ni kwamba mfadhili huwa hagusi madaraka ya viongozi, Wanachama wachezaji, inakuaje yeye anaongea na wachezaji ilhali wachezaji wanatakiwa kuzungumza na kiongozi au mwanachama kambini bila yeye kuwepo huku wakihoji kuwa Manji ni nani ndani ya Klabu.“Leo unatuletea Katibu wa kukaimu ndani ya Yanga toka nje ya uongozi , hivi katiba ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) Inasema Katibu ni wa kuajiriwa au wa kukaimu?”,
Alihoji kuwa Katibu wa kukaimu ana mamlaka gani ya kusaini karatasi za Yanga ambapo alisema hawatatambua nyaraka zozote atakazo saini Katibu huyo, pia ikiwa ni sababu ya kusaini mikataba feki kama alivyowahi kusaini mikataba kama hiyo na Francis Kifukwe Desemba 20 mwaka jana. Klabu hiyo imekuwa ikikumbwa na migogoro mbalimbali toka mwaka huu uanze ikiwa pamoja na kutimka kwa Viongozi wa nafasi mbalimbali ikiwamo ile ya Kaimu Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako, Kocha Mkuu Mserbia Costadic Papic wakiwa na shutuma za kula fedha za usajili wa wachezaji, kupigwa na kuvunjiwa kioo cha gari la Makamu wa rais Mosha wakati wa mechi kati ya majimaji iliyochezwa Jumamosi mjini Songea.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
1 hour ago
0 Comments