Social Icons

Friday, January 28, 2011

BABA YA MUZIKI MSONDO NGOMA WAPATA PIGO

Mwanzmziki Hamisi Maliki Super Maliki kulia akiimba enzi za uai wake kushoto ni Romani Mng'ande na Shukuru Majaliwa (Picha na Rajabu Mhamila).

Na Juma Kasesa
Mwimbaji nyota wa bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ Hamis Maliki (40) amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam, kutokana na maradhi ya kifua yaliyokuwa yakimsumbua muda mrefu.
Akithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo jana, jijini Dar es Salaam, Kiongozi mwandamizi wa bendi hiyo, Saidi Mabera, alisema, Maliki alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu huku akipata matibabu na kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya Msondo.
Alisema mwanamuziki huyo alizidiwa juzi usiku na kukimbizwa katika Hospitali ya Anglikana iliyopo Buguruni Malapa jijini, na kubainika kuwa alikuwa pia na upungufu wa damu, lakini wakati madaktari wakifanya jitihada za kuokoa maisha yake akafariki saa nane usiku wa kuamkia jana.

Alisema mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa ndugu zake Kiwalani jijini tayari kwa mazishi ambayo huenda yakafanyika leo.
Kwa miaka ya hivi karibuni Msondo imekuwa ikikumbwa na misukosuko ya kuondokewa na wanamuziki wake tegemezi ambapo ilianza kwa kumpoteza Selemani Mbwembwe, Athumani Momba, TX Moshi Wiliam na Joseph Maina
.
Mwisho.
MAREHEMU HAMISI MALIKI KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE.
Mwanamziki wa bendi ya msondo ngoma Music ,Hamisi Maliki 'Super Maliki' picha ndogo amefaliki Dunia mwanamziki huyo aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza amefaliki katika hospital ya Agrikan Malapa Dar es salaa alfajiri ya kuamkia leo akisumbuliwa na limonia mazishi yatafanyika kesho mwanamziki huyo aliyejiunga na kundi hilo mwanzoni mwa mwaka 2010 alikuwa akiimba nyimbo za sauti ya kwanza

No comments:

 
 
Blogger Templates