Akizungumzia kuhusu utitiri wa bendi zinzzoundwa na wasanii kutoka DRC hapa nchini amesema wako hapa katika kutafuta masiha na kwamba Kongo kuna wasanii wengi na bendi nyingi nyingine hazisikiki.
Bozia ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki huku akisema atawakumbushia enzi za miondoko ya Nzawise na kusisitiza kwamba anashangaa kuwa Watanzania bado wanazikumbuka nyimbo zake za zamani ilhali ana albamu zingine kadhaa mpya na kuitaja moja yenye jina la ‘Financial Crisis’ yenye ngoma 12 huku akizisifia kwamba zote ni moto wa kuotea mbali.
Aliongeza kwa kusema kuwa alishangazwa kuona kwamba hata alipokuwa katika ziara ya kimuziki nchini Zambia alikuta wanashabikia albamu zilizotoka mika minne nyuma.
Siku ya Jumamosi atatoa burudani katika maskani ya bendi ya Twanga Mango Garden Kinondoni pamoja na wenyeji wao.
Asha aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumapili kundi hilo litajivinjari katika viunga vya Leaders Club ambapo bendi ya Twanga International huwa inatumbuiza katika bonanza kila siku ya Jumapili.
Kiingilio katika maonyesho ya Club Sun Ciro na Mango Garden kitakuwa sh.10,000 na Leaders itakuwa sh 5,000.
0 Comments