Baada ya kuwasili nchini Ijumaa iliyopita akitokea Zambia msanii Aboubakar Bozi Boziana, siku iliyofuata nikawa mwanahabari wa kwanza kufanya naye mahojiano maalum yatakayochapishwa katika Gazeti la Tanzania Daima hapa tukisalimiana kwa cheko na bashasha, hakika nilifurahu kukutana naye ana kwa ana na nilimwambia hilo naye akafurahi kukutana na mimi licha ya kuwa Lugha ilikuwa mushkeli kidogo kwani yeye anaongea Lingala na aliyekaa katikati ni Jerry Kozanga ambaye ni mwanahabari aliyekuwa mkalimani wetu siku hiyo.Kwa ufupi tu msanii huyu ni wa Kimataifa kwelikweli.
Hapa Bozi Boziana akinipa hadithi ndefu ya maisha yake katika muziki tangu alipoanza hadi alipo sasa ambapo tulionge a kwa muda wa masaa 3 hakika yaliyojiri siku hiyo yatwakuwa hadharani siku ya Ijumaa Novemba 26. Natambua wanahabari hapa nchini tuko wengi lakini hata kama wengine wataandika poa tu ni matumaini yangu kuwa kila mtu ana kona yake.
0 Comments