KUMEKUCHA KOMBE LA TUSKER

Kombe hili ndilo litakaloshindaniwa na timu 12 katika michuano ya itakayoanza Novemba 27 2010 , timu hizo na makundi yake ni Kundi A:Tanzania , Zambia, Burundi na Somalia.Kundi B:Rwanda, Ivory Coast, Sudan na Zanzibar na Kundi C:Uganda, Kenya, Malawi na Ethiopia.Mbali na Kombe la CECAFA Tusker Challenge pia timu itakayoshinda itapata zawadi ya Dola 30,000 za Kimarekani(US$30,000), mshindi wa pili atapata dola za Kimarekani 20,000 (20,000 US$) na mshindi wa tatu atapata dola 10,000 za Kimarekani(10,000US $).

Ofisa Habari wa CECAFA Finy Muyeshi katikati , kushoto ni Imani wa SBL hapa wakizungumza na wanahabari hawapo pichani katika Clinic iliyohusu michuano ya Tusker 2010.



Waamuzi 15 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), wameteuliwa kuchezesha michuano ya Tusker Challenge Cup itakayoanza kutimua vumbi Novemba 27 jijini Dar es Salaam na kesho wanatarajiwa kushiriki mtihani wa Copper utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa CECAFA, Finny Muyeshi, alisema kati ya hao waamuzi wasaidizi ni wanane na idadi inayobakia ni waamuzi wa kati.
Muyeshi aliwataja waamuzi wa kati na nchi wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Issa Kagabo (Rwanda), Ressas Librato (Sudan), Israel Nkongo (Tanzania), Dennis Bate (Uganda), Kibo Ibada (Zanzibar), Thomas Onyango (Kenya) na Bamalack Tesseme (Ethiopia).
Waamuzi wasaidizi ni Charles Nizigiyimana (Burundi), Bashir Olad Arab (Somalia), Genreselasie Solomon (Ethiopia), Eleyes Wamalwa (Kenya), Feondagiyimana (Rwanda), Hamas Chang’walu (Tanzania), Hussein Bugembe (Uganda), na Mudani Mustafa (Sudan).
Aidha, Muyeshi aliongeza kuwa, kesho CECAFA itafanya mkutano wa maandalizi ya mashindano ya CECAFA ya mwakani na nchi yatakapofanyika, mkutano utakaofanyika katika Hoteli ya Paradise.
Kwa upande wa timu shiriki, ofisa huyo alisema zitakuwa zikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru na Karume, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mashindano ya TFF, Saad Kawemba, alisema timu za nchi nyingi shiriki katika mashindano ya mwaka huu zinatarajiwa kuwasili nchini leo, ambako hadi kesho zote 12 zitakuwa zimewasili jijini.
Kawemba alitaja hoteli zilipofikia timu za nchi hizo shiriki ni pamoja na wenyeji Tanzania Bara watakuwa Atriums, viongozi wa CECAFA watakuwa Paradise, huku Rwanda, Sudan na Ivory Coast zitafikia Tansoma.
Hoteli ya Landmark kutakuwa na nchi za Uganda, Kenya, Malawi na Ethiopia; Hoteli ya Tanson itakuwako Somalia, wakati Burundi, Zambia na Zanzibar zitakuwa Hoteli ya Johannesburg, wakati waandishi wa nje watakuwa Spices na Hoteli ya Wanyama itakuwa ni kwa ajili ya nchi nyingine shiriki.
Vituo vya runinga vilivyopewa haki ya kuonyesha mashindano ya mwaka huu ni pamoja na Super Sport na TBC, ambavyo vitaonyesha moja kwa moja ‘live’.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Sunday Kayuni akizungumza kwa niaba ya Shirikisho huku akisisitiza Watanzania kutoa sapoti kwa timu ya hapa nchini huku akisema 'Mcheza Kwao Hutunzwa, huku akizitakia michuano yenye heri timu zote.

Aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Kanali Mstaafu Alhaji Idd Kipingu akikabidhiwa Kombe na Mkurugenzi Masoko wa Tusker Caroline Ndungu hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya New Afrika Dar es Salaam.
Meza kuu kutoka kulia ni Meneja Kampeni wa Malaria No More (United Against Malaria) David Kayne,akifuatiwa na Mkurugenzi Masoko Tusker Caroline Ndungu, Mkurugenzi Mahusiano na Uhusiano Mwema katika Kampuni ya Serengeti Breweries TeddyHollo Mapunda,Kanali Msaafu Alhaj Idd Kipingu ,Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye , Mwenyekiti wa Michezo Abdighali Said na Kaimu katibu Mkuu TFF Sunday Kayuni.
Mkurugeni Mahusiano na Uhusiano Mwema SBL TeddyHollo Mapunda, Mkurugenzi Masoko Tusker Caroline Ndungu na Kanali Mstaafu Alhaj Idd Kipingu akipokea Kombe.




Baadhi ya Wanahabari waliokuwepo katika mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments