Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim ‘Sir Nature’, Jumapili hii anatarajiwa kukamua kwenye Ukumbi wa Club Bilicanas katika usiku uliobatizwa kwa jina la ‘Bongo Starz Nite’.Sir Nature aliwataka wapenzi wake na wale wa muziki wa kizazi kipya kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupata burudani ya uhakika kama kawaida yake.Nature alisema, siku hiyo amewaandalia nyimbo mpya ambazo zitaanza kupigwa ukumbini humo, pamoja na shoo ya aina yake.Alizitaja baadhi ya nyimbo mpya atakazozipiga siku hiyo kuwa ni ‘Kwa Muda’ na ‘Part la Kijanja’ alizotamba kuwa ni funika bovu kutokana na jinsi zilivyoandaliwa.Msanii huyo ambaye mambo yake jukwaani yanakubalika kwa mashabiki lukuki wa muziki wa kizazi kipya, safari hii ndiye mwalikwa katika usiku huo maarufu kama Bongo Starz Nite
WATU WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MADAI YA KUHARIBU,KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA
RELI YA KISASA (SGR)
-
WATUHUMIWA Watano Wakiwemo Raia Wa China Wawili Wanaokabiliwa na Tuhuma
za Kuharibu Miundombinu Ya Reli Ya Kisasa (SGR) Wamepandishwa Kwa Mara
ya p...
5 hours ago
0 Comments