Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba Syller Said Mziray amerudishwa hospitalini baada ya hali yake kubadilika ghafla jana.
Kocha huyo ambaye awali alikuwa amelazwa katika hospitali ya Regency kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani ,kwa sasa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU),katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam hiyo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Habari hizo za kulazwa ICU zimekuja mara baada ya uvumi ulioenea jana asubuhi kwamba Super Coach amefariki dunia lakini habari hizo zilikanushwa vikali na vuiongozi wa Klabu ya Simba.
Aidha juzi mchana baadhi ya waandishi wa habari za michezo walikwenda nyumbani kwa Mziray Tabata, Jijini Dar es Salaam kwa nia ya kujua ukweli wa taarifa na uvumi ulionea juu ya hali ya kocha huyo lakini hawakupata ushirikiano wa kutoka na kuishia kufukuzwa na jamaa wa karibu wa Mziray.
KOROSHO TANI 401,000 ZENYE THAMANI YA SHILINGI TRILION MOJA ZIMEZWA NA
KUNUNULIWA
-
Na Ahmad Mmow.
Wakati msimu wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2024/2025 ukikaribia
kumalizika. Mpaka sasa tani 401,000 za korosho zenye thamani ya shilingi ...
1 hour ago
0 Comments