RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajiwa kuongoza maelfu ya Watanzania kuishangilia timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, katika mechi ya kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali ya Mataifa ya Afrika (CAN) dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kuwatembelea katika kambi yao, Naibu Waziri Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa Rais Kikwete anakwenda kushuhudia mechi hiyo kama mgeni rasmi hivyo wanajukumu la kumpa raha ya ushindi sambamba na Watanzania.
“Mechi zote za Stars ambazo Rais Kikwete amekuja uwanjani alikuja kama mshabiki wa soka, lakini hii ya kesho (leo) anakuja kama mgeni rasmi hivyo mtambue mnajukumu la kumpa raha pamoja na watanzania kwa kuibuka na ushindi,”alisema Bendera.
Aliwataka wachezaji hao kucheza kwa kujituma kwa kuzingatia mafunzo waliyopewa na benchi la ufundi na kutoihofia Morocco kwakuwa wanacheza wachezaji 11 kama ilivyo kwa Stars.
“Hakuna sababu ya kuhofia majina ya wachezaji wao hata kama wanacheza soka ya kulipwa Ulaya, kwani tayari mmeshacheza na Algeria na timu nyinginezo zenye wachezaji wenye majina makubwa na mkafanya vizuri,naamini mnaweza kuibuka ushindi hasa mkizingatia mnacheza nyumbani,”alisema Bendera na kuongeza. “Lakini mnapaswa kufahamu kuwa mcheza kwao hutunzwa, ni jukumu lenu kuhakikisha mnawagaragaza Morocco kwakuwa watanzania wapo nyuma yenu kuwashangilia,” Aliwaambia kuwa katika kundi lao kila timu ni nzuri na inayotakiwa kufuzu ni moja, hivyo watambue Stars ndiyo timu pekee inayotakiwa kufuzu ili kucheza fainali hizo ambazo zimepangwa kufanyika Equatorial Guinea na Gabon 2012 na kuwataka mashabiki wa soka wa jijini la Dar es Salaam na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo katika muda wote wa dakika 90.
Bendera aliwataka wachezaji kutambua kuwa wanatizamwa na ulimwengu mzima kwakuwa mechi hiyo itaonyeshwa na kituo cha Televisheni cha Supersport, hivyo ni nafasi yao kujitangaza kwa kuonyesha soka ya kisasa ili kuweza kununuliwa na klabu mbalimbali duniani.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA UKIMWI YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA AFUA
ZA UKIMWI NJOMBE
-
NA. MWANDISHI WETU – LUDEWA
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI,
Mheshimiwa Dkt. Elibariki Kingu ametoa piongezi kwa M...
3 hours ago
0 Comments