Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Ghonche Materego katikati Kiongozi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta ' Luiza Mbutu na Mwanahabari Hassan Bumbuli. Leo asubuhi walikuwa na mkutano wa Jukwaa la Salaa ambao hufanyika kila siku ya Jumatatu BASATA,Ilala Dar es Salaam.Aidha Luiza amekiri kwa kusema kuwa wasanii wa kike wataendelea kudhalilishwa na jamii hivyo amewataka wanajamii kutofautisha sanaa na mavazi .Alisema hayo wakati alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa watu waliohudhuria kwanini wacheza shoo na wanamuziki wa kike wanapeenda kuvaa mavazi yasiyostahili. Nyeye alijibu hivi:Ni kweli tubnapata lawama nyingi na sisi tunazikubali lakini pia ikumbukwe kwamba hata mashabiki nao ni wahuni , nakumbuka wakati nilipokuwa mjamzito tena mimba ya miezi 9 mashabiki na wapenzi wangu walikuwa wakija kunitunza pesa kwa kuniwekea katika matiti ilhali mkono wangu upo. Kadhalika hata hao wacheza shoo wakivaa nguo ndefu kama magauni na kufunga mikanda bado mtu akienda kuwatunza ataweka pesa yake katika kiuno au makalio hivyo mambo hayo hayakwepeki licha ya kuwa sisi wasanii wa kike hatupendi kuwafanyiwa hivyo.Kama hiyo haitoshi Luiza ametolea mfano wa ngoma za kienyeji kwa kusema kuwa anakumbuka hata alipokuwa mtoto ambapo yeye alikuwa akicheza ngoma shuleni walikuwa wakifungwa khanga walivuliwa mashati na kufungwa khanga kifuani huku tumbo na mgongo vikibaki wazi .Wakati huo huo alimalizia kwa kusema kuwa hawezi kuihama bendi ya Twanga Pepeta kwa sababu yeye na Jesca Charles walikuwa miongoni mwa wasanii waanzilishi na waliishi katika maisha magumu kiasi kwamba yeye alikuwa akiiba chakula nyumbani kwao na kupeleka katika kambi ya Twanga wanapika na kula sasa haoni sababu ya kuhama hivi sasa wakati ikiwa ina mafanikio na yeye ni mmoja wa walioijenga bendi hiyo labda ife hapo ndipo atatafuta bendi nyingine.
0 Comments