MGAMBO KUSAIDIANA NA ASKARI POLISI KULINDA USALAMA KATIKA VITUO KWENYE UCHAGUZI MKUU UJAO

Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamesema watawatumia Askari Mgambo ikiwa ni njia moja ya kusaidiana na Jeshi la Polisi kulinda Usalama wa vituo wakati wa zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Wakurugenzi hao waliyasema hayo wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa mitatu ya Kanda ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wametoa wito kwa kila askari mgambo kupiga ripoti kwa mshauri mgambo wa wilaya yake.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Bw. Gabriel Fuime, na Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke Bw. Stephen Kongwa, wamesema kuwa mgambo hao watakuwa sehemu ya walinzi wa vituo pia watalipwa posho kama ilivyotagazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wamesema Mgambo hao watahakikiwa na kupangiwa kazi na baadaye kutagawanywa katika vituo watakavyopangiwa na Wakurugenzi katika Halmashauri husika.

Post a Comment

0 Comments