Aliyekuwa mwakilishi wa shindano la Big Brother Africa All Stars Mwisho Mwampamba anatarajiwa kurudi nchini saa moja usiku wa leo hiyo ni kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano mkuu wa Multichoice Tanzania inayosambaza ving’amuzi vya Dstv nchini, Barbra Kambogi alisema kuwa, Mwisho anatarajiwa kurudi akitokea katika shindano hilo na kufanikiwa kuingia tano bora huku akiambulia nafasi ya nne.
Barbra alisema kuwa kwa kuonyesha uzalendo aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumpokea uwanja wa ndege kutokana na kupeperusha bendera ya Tanzania nchini Afrika kusini.
“Nawashukuru Watanzania kwa kushirikiana naïf muda wote kwa mshiriki wetu alipokuwa akishiriki kwenye jumba BBA, tunajisikia faraja kwa kukaa siku zote 91, na kufikia nafasi ya nne, tujitokeze kwa wingi kumpokea” alisema Barbara.
Aidha, Barbara alisema kuwa kutakuwa na gari maalum litakaloanzia Posta eneo la Idara ya Habari Maelezo majira ya saa 11 jioni hadi saa 12 ; 15, kisha kuelekea uwanja wa ndege na kumlaki sambamba na kuongea na waandishi juu ya mambo aliyojifunza huko na mipango yake ya baadae.
Katika fainali hizo zilizomalizika siku ya Jumapili, mshiriki wa Naigeria, Uti aliweza kunyakua kitita cha dola 200,000 za marekani kwa kuwabwaga washiriki wenzake waliyoweza kudumu humo kwa siku zote 91, akiwemo Mzimbabwe, Munya ambaye alishika nafasi ya pili, huku Lerato (Afrika kusini) akishikanafasi ya tatu sambamba na Mwisho nafasi ya nne na Mkenya Sheila kushika nafasi ya tano.
0 Comments