JE WAJUA KWAMBA ASALI YA ITIGI INAONGOZA KWA UBORA


Na Mwandishi Wetu , Itigi Manyoni.

Mzee Abel Mdinka kulia akiwa ameongozana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini Kapteni John Chiligati wakati alipotembelea Shamba la Nyuki la Maua lililopo katika kijiji cha Mwanzi Manyoni hivi karibuni kulia nyuma ni Timothy Abel Mdinka Mkurugenzi Mtendaji wa Maua.

Katika pitapita yangu mkoani Singida nilikutana na Mkurugenzi wa Manyoni Asili Utilization Apiary (Maua) Bw. Timothy Abel Mdinka ambaye anamiliki shamba kubwa la nyuki mkoani huo akishirikiana na baba yake mzee Abel Mdinka akanisimulia ni jinsi gani walifanya na kuamua kuanzisha shamba hilo kubwa.

Timoty alianza kwa kusema Manyoni Asili Utilization Apiary (MAUA), ni Shamba la ufugaji nyuki ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Manyoni, lina ukubwa wa ekari 216 ambayo inajumuisha banuai ya pekee duniani , banuai yenye uoto wa asili wa Itigi Thichets hupatikana sehemu mbili tu katika uso wa dunia nayo ni Manyoni na Zambia.

Uoto huu wa asili unaotengeneza maua ya pekee unawezesha nyuki kupata asali yenye ubora wa hali ya juu na pekee kabisa duniani, mpaka sasa asali ya Itigi ndiyo asali bora zaidi kupita zote na ilipata ushindi wa kishindo katika maonyesho ya asali yaliyofanyika mwaka jana pale Mnazi mmoja.

Nia na madhumuni ya kuanzisha mradi huu ni 1.MAUA tunataka kutunza msitu huu wa pekee duniani .

2.MAUA tunataka Kuwa mfano bora na wakuigwa na jamii inayotuzunguka katika utaunzaji wa mazingira na kufuga nyuki.

3. MAUA tunataka kutumia mali asili ya pekee duniani tuliyopewa na Mungu katika kupunguza umasikini na kutunza mazingira .

4.MAUA tunataka kufanya mradi wa kufuga nyuki uwe mradi mbadala wa kiuchumi ambao utasababisha watu waache kuuza mkaa na na wafuge nyuki ambayo ni sehemu ya kutunza mazingira.

5.MAUA tunataka kuitangaza Manyoni Kitaifa na Kimataifa ili tuweze kufungua soko la asali na bidhaa zake. Mradi huu ulianza mwaka 2006 chini ya uongozi wa Mzee Abel Mdinka na Kijana wake Timothy Mdinka, uamuzi huu ulitokana na hali halisi ambayo mzee mdinka amakuwa akiiona ikiendelea kutokana na jinsi ambavyo misitu inakatwa kwa ajili ya maendeleo ya binadamu na kuanzisha mashamba pamoja na ufugaji mifugo usiozingatia utunzaji wa mazingira.(Habari na http://www.fullshangwe/.blogspot.com.

Post a Comment

0 Comments